Header Ads Widget

WAZIRI WA ARDHI ASIFU MIAKA MINNE YA RAIS DKT SAMIA

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi nchini Tanzania,  Deogratius Ndejembi amesema ndani ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, mapinduzi makubwa yamefanyika kwenye sekta ya ardhi nchini sambamba na uwezeshaji mkubwa uliofanikisha maendeleo na maboresho makubwa kwenye sekta hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sera ya ardhi ya mwaka 1995 toleo la mwaka 2023, Jijini Dodoma kwenye kituo cha mikutano cha Jakaya Kikwete Dodoma, Mhe. Ndejembi amesema maelekezo ya Rais Samia ya kuhakikisha wanapanga na kupima ardhi yamefanyika kikamilifu kuliko wakati mwingine wowote ambapo takribani Bilioni 50 zimetolewa na serikali, Wizara ya ardhi na TAMISEMI ikifanikiwa kuzikopesha Halmashauri zaidi ya 52 kwaajili ya upimaji ardhi.

Aidha Serikali ya Rais Samia pia iliridhia na kutoa Bilioni 133 kwaajili ya vitendea kazi mbalimbali vya kuboresha sekta ya ardhi nchini, ambapo kati yake fedha hizo zimewezesha kununua magari 70 ambayo hii leo yamekabidhiwa kwa Wizara hiyo na Rais Samia Suluhu Hassan.

Aidha wakati wa kukabidhi tuzo kwa Rais Samia ya kutambua mchango wake katika usimamizi wa mifumo ya sekta ya ardhi, Waziri Ndejembi pia amesema Serikali ya awamu ya sita pia ndani ya miaka minne ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, imetoa Dola za Marekani Milioni 65 ambazo zimetumika kutengeneza ramani msingi mpya ya nchi suala ambalo kwa mara ya mwisho lilifanyika mwaka 1978.

Post a Comment

0 Comments

MAGAZETI

NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI