Dr Nice akimfanyia mtoto aliye tumboni uchunguzi wa magonjwa ya moyo
Wananchi wakisubiti kupata huduma
NA NAMNYAKI KIVUYO, ARUSHA
Kati ya wajawazito 91 waliofanyiwa uchunguzi wa magonjwa Moyo mkoani Arusha kuelekea siku ya wanawake Duniani watano wabainika kuwa na watoto wenye magonjwa hayo tumboni.
Hayo yalielezwa na Daktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete Dkt nice Majani wakati akiongea na waandishi wahabari mkoani sha ambapo alisema kuwa kwa muda wa siku tano wamweza kuwaona wagonjwa 301 kati yao wajawazito ni 91, watoto 70 na watu wazima 140.
"Tumeweza kufanya uchunguzi wa magonjwa ya moyo kwa watoto kabla ya kuzaliwa na tumegundua wamama watano wana watoto wenye matatizo ya moyo ya kuzaliwa ambapo tumeshapanga watazalia katika hositali gani na tumeshachukua taarifa muhimu ambapo watakapo zaliwa watafanyiwa tena uchinguzi na kuanza matibabu kwa haraka, Dkt Majani.
Aidha alieleza kuwa magonjwa ya moyo kwa watoto yamegawanyika kayika makundi mawili ambapo ni magonjwa ya kuzaliwa pamoja na yanayokuja baadae lakini katika kliniki yao ya moyo wameona asilimia 75 ya magonjwa hayo ni ya kuzaliwa ambapo takwimu za Dunia inaonyesha kila watoto 100 wanaozaliwa hai mtoto mmoja ana tatizo la moyo.
"Sababu zipo nyingi mojawapo ni katika ile miezi mitatu ya ujauzito wakati moyo ndio unatengenezwa mama akipata maambikizi na akaumwa na homa kali, lishe duni, kukosa virutubisho muhimu (Folic acid) ambayo mama anatakiwa kutumia miezi sita kabla ya kubeba ujauzito,"Alieleza.
"Wengi wameanza kunywa Folic acid mwezi mmoja mpaka minne baada ya kuwa na ujauzito na wakati huo moyo unakuwa umeshatengenezeka ambapo kama kuna kasoro tatizo linakuwa limeshatokea lakini pia sababu nyingine ni kunywa pombe kwa mama mjamzito na kuvuta sigara na hapa kwenye sigara ni aidha mama, baba au mtu anayemzunguka na kikibwa zaidi ni vinasababu wengine wanarithi," Alifafanua.
Aliendelea kusema kuwa sababubu nyingine ni matumizi ya dawa zozote kwa muda mrefu na kutolea mfano wamama wenye Presha au sukari na wanatumia dawa kabla ya ujauzito na wakati wa ujauzito kuna uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto wenye ugonjwa wa moyo.
Kwa upande wake Dkt Engarasia Kifai daktari bingwa wa magonywa ya moyo kwa watu wazima kutoka taasisi hiyo alisema kuwa mwamko wa wananchj umekuwa ukiongezeka ambapo kwa upande wa wanaume ugonjwa wa mgandamizo wa moyo ndio umekuwa mkubwa kwao na nyingine ni kutanuka kwa misuli ya moyo kwa wanawake na wanaume pamoja na mishipa ya damu ya kwenye moyo kuziba ambayo tumepata kwa wanaume wawili na mmoja shambulio la moyo la hatari.
"Kuziba kwa mishipa ya damu ya moyo inaweza ikachangiwa na kuwepo lwa shinikizo kubwa la damu, kuwepo na lehamu nyingi, uzito kupindukia, uwepo wa ugonjwa wa kisukari, kutofanya mazoezi, utumiaji wasigara ,"Alieleza.
0 Comments