Profesa Sarungi enzi za uhai wake
Na Andrew Chale, Dar.
ALIYEWAHI kuwa Waziri wa zamani katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Profesa Philemon Sarungi (pichani juu) amefariki dunia leo Machi 5, 2025.
Kwa mujibu wa taarifa iliyobandikwa katika mitandao ya Kijamii kupitia kwa Maria Sarungi mmoja wa watoto wa Mwanasiasa huyo mkongwe, imenukuu taarifa ya msemaji wa familia, Martin Leonard Obwago Sarungi.
Katika taarifa hiyo, imebainisha kuwa, Profesa Sarungi amefariki Majira ya saa 10, jioni na msiba upo nyumbani kwake Mtaa wa Oysterbay Mtaa wa Msasani, huku taratibu zingine zikitarajiwa kutolewa hapo baadae.
0 Comments