Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imewapokea wataalamu 10 kutoka Chuo Kikuu cha St. Petersburg, Russia, waliowasili nchini leo kwa ajili ya ziara ya kubadilishana ujuzi na teknolojia katika sekta ya misitu.
Ziara hii ni sehemu ya ushirikiano wa kimkakati kati ya Tanzania na Russia katika uhifadhi wa misitu na maendeleo ya sekta hiyo.
Ushirikiano huo ulianza kufuatia maelekezo ya Mheshimiwa Waziri Mkuu baada ya kikao cha Wakuu wa Nchi za Afrika na Russia mwaka 2023.
Kwa muktadha huo, taasisi za TFS, TAFORI, na SUA zimehusika katika maandalizi ya makubaliano hayo, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kitaaluma na kiutafiti kati ya nchi hizi mbili.
0 Comments