Header Ads Widget

WANAVYOMJUA BASHE NJE YA NZEGA SIVYO ALIVYO NDANI

(Pichani Hussein Bashe akiwa na vazi la asili Jimboni Nzega Mjini -Picha kwa hisani ya Mtandao).


Viongozi wengi wa kisiasa huwa wanajitengenezea taswira fulani ktk uongozi wao.

Kwa mfano aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Sokoine, alijijengea taswira inayofanana kidogo na taswira ya wayahudi (wana wa Israel), taswira ya uchapa kazi na ushujaa dhidi ya mafisadi, kwa wakati huo wa Sokoine yakiitwa "wahujumu uchumi".

Rashidi Kawawa aliyekuwa Waziri Mkuu, alijijengea taswira kama mmoja wa viongozi watiifu sana mbele ya Rais, Mwalimu Nyerere, kiasi cha kutenda lolote analoagizwa na Rais Nyerere wakati mwingine bila uelewa wa kina - mfano utekelezaji wa oparesheni vijiji (vijiji vya ujamaa).

Dk. Salim Ahmed Salim, Waziri Mkuu wa nne wa Tanzania, alijijengea taswira ya kiongozi anayejiheshimu na muungwana.

John Malecela, aliyekuwa Waziri Mkuu, alijijengea taswira ya kuwa Waziri Mkuu mtata, mwenye kauli kali wakati mwingine bila kupima athari zake mbele ya umma.

Ikumbukwe aliwahi kushauri wananchi wa eneo fulani hapa nchini wahifadhi pumba ili wazitumie kama chakula nyakati za ukame (njaa).

Sina maana ya kuwaelezea mawaziri wakuu wote wa Tanzania hapa, lakini najaribu kujenga hoja yangu kwa kuonesha viongozi mashuhuri wa ngazi ya juu waliowahi kujijengea taswira fulani.

Na kwa kuwa viongozi hao wamelitumikia taifa letu ni rahisi kunielewa ninachotaka kusema au kumaanisha hapa.

Nayasema haya kwa ukweli na uwazi, kwa nia njema na kwa maslahi ya Wilaya yetu na taifa letu kwa ujumla.

Ukweli ni msingi wa lazima, na kwa kweli ukweli ni uadilifu kwa sababu unapaswa kuzijenga dhamiri zetu ili kumsaidia mwanadamu kupata mwanga unaofukuza mikanganyiko.

Katika jamii isiyojali ukweli, uhuru, inapoteza msingi wake na mwananchi anakuwa mhanga wa vurugu na kutawaliwa kwa hila. (Efeso 4:15, 1 Korinto 13:6, Mithali 23:23).

Mbunge wa jimbo la Nzega Mjini, Hussein Bashe, naye amejijengea taswira yake, lakini ni taswira inayokanganya.

Kwa namna fulani Bashe anaonekana kama ni mwanasiasa mahiri sana ktk kufikiri tofauti, huko nje ya Nzega wengi wanamfahamu kama mtu makini, mwenye mapenzi mema na wananchi, yaani kwamba ni mwanasiasa bora kuwahi kutokea ktk medani ya siasa za Tanzania.

Mkanganyiko mwingine unaojitokeza kwenye taswira ya Bashe na ambao wengi hawamjui vema ni kwamba Bashe ni kiongozi anayeweza kutumia madaraka yake kutisha watendaji serikalini pamoja na watu wanaowaza tofauti na yeye.

Bashe ni dikteta, mnafiki, mfitini, mchonganishi, fisadi, mwongo, si mwaminifu na asiyefaa kuingoza hata genge la wahuni.

Jana Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefika Wilaya ya Nzega kufungua Stand ya Mabasi, lakini amefungua Stand ambayo haijakamilika "..yenye mapungufu".

Mapungufu hayo ukilinganisha na fedha iliyotolewa na serikali (Bilioni 4.2) unapata na mashaka makubwa.

Stand iliyotumia Bilioni 4.2, imejengwa chini ya kiwango na bado inamapungufu makubwa.

Mbio za mwenge zilizofika Wilayani Nzega, kwa mara mbili zinagomea kufungua Stand hii kutokana na ufisadi uliofanyika, Rais wa nchi naye aligomea kufungua Stand hiyo kutokana na sababu zile zile.

Mbunge w jimbo hili, Hussein Bashe, aliwahi kuingia mgogoro na Mkurugenzi (Magesa) wa Halmashauri ya Mji wa Nzega juu ya ujenzi wa Stand hii ya Nzega, Mkurugenzi na wataalamu pamoja na baadhi ya Madiwani walipendekeza na kutaka ujenzi wa Stand ufanywe na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na wakatoa sababu ya msingi kwamba hawa jamaa " JKT" hawanaga cha kuchakachua, wanajenga kwa kiwango na kwa wakati.

Lakini Mbunge kwa maslahi yake binafsi aling'ang'ania mkandarasi wake ili afanye yaliyokuja kutokea sasa, Stand imejengwa chini ya kiwango na kuwa yenye mapungifu, ukifika pale ni kichekesho unapoilinganisha Bilioni 4.2 na kilichofanyika!

Jana wakati wa ufunguzi, Waziri Mkuu alitaka taarifa ya jimbo la Nzega Mjini juu ya matumizi ya fedha iliyotolewa na serikali (Bilioni nne na pointi mbili) zimetumikaje ktk ujenzi wa Stand hiyo!

 Cha kushangaza ni kwamba Mbunge Hussein Bashe ambaye ndiye alikuwa mwenyeji, hakuwepo, wala Katibu wake Mbunge wa jimbo naye hakuwepo!

Maana yake Waziri Mkuu hakupokelewa na mwenyeji, ambaye ndiye alipaswa kuonesha kazi yake ya kibunge kwenye miradi mikubwa kama hii  ya Stand wananchi wajue Bilioni 4.2 amezisimamiaje Mbunge wao?

Unaweza kusema hii ni dharau, ni udhaifu mkubwa uliofanywa na Mbunge pamoja na ofisi yake kwa ujumla.

Hili ni moja tu kati ya mambo ya hovyo anayoyafanya Mbunge Hussein Bashe, baada ya mbio za mwenge kukataa mara mbili kuifungua Stand, na Rais kugomea, Bashe aliona anakwenda kuumbuka mbele ya wananchi, akaanza kuwatwisha lawama watendaji wa serikali na madiwani, na kwa kuwa anawatishia nafasi zao, walikaa kimya.

Huyu na ufisadi wake huo, ni wa mitano tena!?

Sitaki kugusia mambo mengine ambako nako ameshindwa, tkutune kwenye uchambuzi wa majimbo ya Nzega, sasa tuko kwenye jimbo la Bukene tunaelekea kuhitimisha.

Lakini niseme tu kwa kweli inasikitisha sana kuiona jamii inavumilia wanasiasa aina hii ya Bashe wanaofanya ufisadi ktk miradi ya umma.

Iko wapi hasira ya wazazi ambao wanachangishwa pesa mashuleni ili kulipa waalimu wa kujitolea wanaowafundisha watoto wao, wakati mbunge anajinasibu kila mara kusomesha watoto wa masikini?


Iko wapi hasira ya vijana wanaoishi maisha duni karibu na mgodi na ambao hawakupewa haki ya kuchimba madini ktk ardhi ya Wilaya yao, badala yake wakapewa wapambe wa Bashe?

Ni jambo la ajabu sana kuona fisadi akishangiliwa na kuonwa kama mungu watu, mzalendo mwenye mapenzi mema na wananchi, yaani kuna watu wanaamini bila yeye hawawezi kuishi wala kufanya maendeleo.

Hakuna utamaduni wa kuchukia ufisadi wala mafisadi hapa Nzega.

Nataka nihitimishe makala yangu kwa kuwaambia wananchi wenzangu, iwe ni wananchi wa Nzega au huko mliko ktk viunga vya Tanzania, kwamba, utamaduni wa kuchukia ufisadi ndiyo uliofanya Denmark kushika nafasi ya nchi bora 10 duniani.

Utamaduni huu ndiyo utakaoikoa Wilaya yetu ya Nzega au  taifa letu la Tanzania.

Ili kujiondoa kwenye makucha ya wanasiasa mafisadi aina hii ya Bashe, wananchi na tume ya maadili, nchi nzima iweke mkakati wa kuwajengea wananchi saikolojia ya kuchukia ufisadi na kuporomoka kwa maadili.

TAKUKURU na jeshi la Polisi wachukie ufisadi na waungane na wananchi wanaopinga dhuluma  na ufisadi.

Idara ya Usalama wa Taifa wachukie ufisadi na washirikiane na wananchi kulinda kodi na rasilimali za nchi ili zitumike vyema kwa maslahi ya nchi yetu.

Wafanyakazi na vijana kote nchini wachukie ufisadi na wasiwapokee wanasiasa - watuhumiwa wa ufisadi waliopo madarakani na wanaotangaza nia ya kuwania ubunge.

Nihitimishe makala hii kwa kutumia utenzi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwamba,

"Ole wake Tanzania tusipoisaidia!

Niwezalo nimefanya; kushauri na kuonya.

Namlilia jalia atumlikie njia; Tanzania ailinde waovu wasiivunde".


Kwiyeya Singu. 0784977072

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI