Header Ads Widget

MGORE MIRAJI,CHIEF KIUMBE WACHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA IJUMAA MUSOMA

Na Shomari Binda-Matukio Daima            Musoma 

MJUMBE wa Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi Taifa Mgore Miraji na mfanyabiashara Muhamed Kiumbe maarufu ( Chief Kiumbe) ni miongoni mwa waumini wa dini ya Kiislam waliochangia ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Musoma.

Kila mmoja baada ya swala ya ijumaa leo machi 14,2025 amechangia kiasi cha shilingi laki 5 na kufanya makusanyo ya jumla ya shilingi milioni 2 na laki 7.

Akizungumza wakati akihamasisha suala la uchangiaji wa ujenzi wa Msikiti huo,mlinganiaji wa dini ya Kiislam kutoka jijini Dar es salam Ally Kadogoo amewapongeza waumini wa dini hiyo mkoa wa Mara kwa kujenga Msikiti mkubwa na wa kisasa kwa michango yao.

Amesema misikiti mingi mikubwa na mizuri kama wa mkoa wa Mara imejengwa kwa ufadhili lakini wa mkoa wa Mara umejengwa kwa michango ya waumini.

Sheikh Ally amesema alikuwa Musoma miaka 3 iliyopita lakini kwa sasa ameona mabadiliko makubwa ambayo waumini wanastahili kupongezwa.

" Nimeshangazwa niko hapa Chief Kiumbe anapigiwa simu yupo Dar anatuma kiasi cha shilingi laki 5 lakini nimeambiwa tangu ujenzi umeanza amekuwa mchangiaji mzuri.

" Nimshukuru pia dada yetu Mgore Miraji naye ametupa fedha taslim shilingi laki 5 kiukweli hii ni jihad kubwa ambayo mnaifanya waumini wa mkoa wa Mara na mnastahili kuombewa dua",amesema.

Kwa upande wake afisa kutoka ofisi ya Katibu mkuu Bakwata makao makuu Burhan Muhamed amesema juhudi za waumini wa mkoa wa Mara kwa ujenzi wa Msikiti huo zinapaswa kuigwa na maeneo mengine.

Shekh wa mkoa wa Mara Msabaha Kassim amewashukuru wageni hao kwa kufika mkoa wa Mara na kuhamasisha masuala ya dini kwenye kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhan



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI