TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII
NA HABARI NA MATUKIO APP
Hali ya usafi wa mazingira katika kituo cha mabasi Mbalizi wilayani Mbeya bado hairidhishi kutokana na kurundikana kwa taka taka katika baadhi ya maeneo ya ndani na nje ya kituo hicho.
Baadhi ya maeneo ya kituo hicho cha mabasi yameshuhudiwa yakiwa bado ni machafu hasa kwenye mitaro ya maji hali ambayo inahatarisha usalama wa afya za wafanyabiashara na wasafiri pia wananchi kwa ujumla.
Halmashauri ya wilaya ya Mbeya, imefika kwenye kituo hicho na katika masoko makubwa ya mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi (Soko A na Soko B Tarafani) kwa ajili ya kuongoza zoezi la usafi katika maeneo mbalimbali ya kituo hicho cha mabasi na masoko hayo mawili ikiwa ni kilele cha juma la mazingira nchini.
Akizungumza kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mbeya Bi. Erica Yegella, afisa mazingira wilayani Mbeya John Rulala, amesema Halmashauri inaendelea kusimamia utunzaji na usafi wa mazingira kwa mustakabali bora wa afya za wananchi na kwamba imeamua kuwatumia viongozi wakiwemo wa wafanyabiashara kuwatangazia wananchi na wafanyabiashara juu ya kujitokeza kufanya usafi, utaratibu ambao wamekuwa wakiutekeleza kila juma mara mbili (jumatano na jumamosi) na kuelekeza viongozi wa vijiji, vitongoji na kata kuendelea kusimamia ipasavyo usafi wa mazingira.
Rulala amesema Halmashauri ina vifaa kwa ajili ya usafi ambapo katika mji wa Mbalizi wanaendelea kuboresha hali ya usafi wa mazingira.
Baadhi ya wananchi wakiwemo wafanyabiashara katika mamlaka ya mji mdogo wa Mbalizi wamesema hali ya usafi inaridhisha kwa sehemu kubwa lakini kwa baadhi ya maeneo bado ni kero hasa kwenye mitaro kutokana na kurundikana kwa takataka hivyo kuwa kero kwa usafishaji hasa kwa wanawake tofauti na hapo awali ambapo kulikuwa kikosi maalum ya kuzibua mitaro.
0 Comments