Header Ads Widget

WANANCHI BONDO WAFIKA DODOMA KUOMBA MSAADA KWA WAZIRI MKUU

 


Na Hamida Ramadhan Matukio Daima App DODOMA

WANANCHI wa kijiji cha Bondo, wilayani Kilindi, Mkoa wa Tanga, wamefika jijini Dodoma kuwakilisha zaidi ya watu 1000 katika juhudi za kuonana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  

Wananchi hao wanadai nyumba zao kuchomwa moto na mazao yao kuharibiwa kwa madai ya kuishi katika msitu wa hifadhi unaomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

Wakizungumza na waandishi wa habari, Daniel Naoki alieleza kuwa hali yao ni mbaya, wakidai kwamba wamejikuta bila makazi na kukumbwa na ghasia.

 "Tumeishi katika eneo hili kwa zaidi ya miaka 50, lakini sasa tunafukuzwa kwa nguvu," amesema Naoki. Eliha Lissu 

Na kuongeza kuwa "Wanakabiliwa na vitisho kutoka kwa viongozi wa Tanga na hawajapata ushirikiano wowote kutoka kwao, " Amesema.

Halima Saidi, mzaliwa wa Bondo, alifafanua kuwa sasa wanalazimika kulala porini bila makazi na chakula, huku wakikabiliwa na hali ngumu ya maisha.

 "Tunahitaji msaada ili tupate mahali pa kuishi na kuendeleza shughuli zetu za kilimo," amesisitiza.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Kilindi, Hamis Mgandila, alieleza kuwa eneo hilo limekuwa hifadhi tangu miaka ya 60 na kwamba wananchi walitakiwa kuondoka baada ya kushindwa mahakamani.

Kwahiyo lilifanyika zoezi tu la kuwaondoa kwenye maeneo hayo Lakini mkuu wa Mkoa wa sasa Batilda Burian alitoa notisi ya siku 14 wakitakiwa kuondoka 

Kikubwa wanatikiwa watii sheria maana yake ni msitu wa hifadhi toka miaka ya 60,

"Na mnatakiwa mjue dunia sasa inakabiriana na mabadiliko ya tabia nchi kwahiyo kama tutaendelea kuathiri hivi vyanzo pamoja na mazingira tafsiri yake kama nchi tunaenda sehemu ambayo inawezekana ikawa ni mtihani yale maeneo ambayo yametengwa kama hifadhi hususani maeneo yale kwahiyo wao walitakiwa kutii sheria tu na kuondoka ,"alisema.

Mbunge wa Jimbo hilo, Omary Kigua, alithibitisha kuwa eneo hilo ni la serikali na kwamba walipata taarifa ya kuondoka.

" Bondo ni hifadhi ya Serikali ipo kwenye kijiji cha Mswaki na Bondo ina GN yake mwaka 61 ni eneo la serikali kwa hao wananchi tena siyo kwa wananchi wa Kilindi hao ni wananchi waliotoka maeneo mengine walio wengi wametoa Manyara,Babati mwanzoni walikuwa wanalima mashamba waliambiwa na watu wa TFS ili eneo lina mita za mraba 11,000 wakaambiwa waachiwe 3,000 wao wakakataa wakaenda wakashitaki Mahakamani mpaka Mahakama kuu mara mbili wameshindwa kesi , " Amese

Ameendelea kuekeza Mbunge wa Jimbo hilo walivyoshindwa kesi mwaka wa juzi wakapewa notisi ya kuondoka kwenye eneo la serikali hilo siyo eneo la wazi ni eneo la serikali lipo chini ya TFS na walivyopewa taarifa hawakuondoka

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Dkt. Batilda Burian, alikiri kuwa suala hilo linasimamiwa na wizara husika na alisisitiza kwamba wananchi wanatakiwa kufuata sheria na taratibu za kuhamia maeneo mengine.

" Ni kweli  eneo hilo  ni la TFS na waliwapa maelekezo Jeshi la wananchi kwajili ya mazoezi kwahiyo suala la jeshi kwenda kufanya hilo zoezi tunalijua, " Amesema

Na kuongeza Hayo mengine yakuchomewa sijapata kuona wala kusikia najua heshima na nidhamu ya jeshi letu hawajawahi kufanya mambo ya uzembe yakifedhuri ndiyo maana hata wanapokwenda katika vikosi vya mazoezi huko Congo wanafanyakazi ya heshima na hawajawahi kulaumiwa kama majeshi mengine yanavyolaumiwa, " Amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI