Header Ads Widget

RC DENDEGO AONGOZA WANAWAKE KUSHIRIKI UJENZI WA SHULE YA AMALI

 


Na Thobias Mwanakatwe,SINGIDA 

KATIKA kuonyesha kuwa wanawake wanaweza,Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, leo (Machi 4, 2025) amewaongoza wanawake wa Wilaya ya Singida kwa ajili ya kushiriki ujenzi wa shule ya amali ya Mkoa wa Singida inayojengwa kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida kwa gharama ya Sh.bilioni 1.6 ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.

Akizungumza na wanawake waliojitokeza kushiriki ujenzi huo amesema halmashauri zote za mkoa huu zimepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya amali lakini katika shule ya amali ya Mkoa watachaguliwa kujiunga wanafunzi wenye vipaji.

"Tunashukru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan tumeona dhamira yako ya kweli kwa Watanzania ya kuweza kuwakwamua kiuchum,shule hii ya amali inatojengwa katanya Unyambwa tutawachagua wenye vipaji ndio wajiunge ili watuletee mageuzi ta kiuchumi,alisema.



Dendego alisema nchi yetu imezindua sera mpya ya elimu inayokwenda kuangalia vitendo na elimu ya nadharia lengo ili mwanafunzi anapohitimu masomo aweze kujiajiri au kuajiriwa akiwa tayari ana ujuzi mkubwa.

Aidha,Mkuu wa Mkoa wa Singida amezipongeza wilaya zote wa mkoa huu kwa kutekeleza maelekezo ya serikali katika kuadhimisha siku ya wanawake dunia kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa ambayo yamewashirikisha wanawake kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.

Awali Mhandisi wa Manispaa ya Singida amesema serikali  imetoa Sh.Bilioni.1.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya amali ya Mkoa wa Singida ambayo itakapokamilika katika awamu ya kwanza itachukua wanafunzi takribani 400 wenye vipaji watakaofindishwa ufundi wa aina mbalimbali.


Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Halima Dendego, ambaye aliongoza mamia ya wanawake wa Wilaya ya Singida kushiriki ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni Machi 8, 2025.

Amesema katika awamu ya kwanza ujenzi ambao unatarajia kukamilika Mei 29, 2025 majengo 22 yatajengwa yakiwamo madarasa nane,maabara 2,mabweni 4,karakana ya ujenzi na ufundi uashi na karakana ya ufundi magari na kuchomelea.


MWISHO

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI