Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Baadhi ya wakulima na wanachama wa vyama vya ushirika vinavyounda Chama kikuu Cha ushirika mkoa Wa Njombe wameutaka uongozi wa NJORECU na Bodi kuchukua hatua za haraka katika kusuluhisha Migogoro kwenye vyama vya msingi vinavyosigana na baadhi ya Wadau na Serikali ili kuokoa mali za ushirika.
Wakulima hao Akiwemo Chrispin Kapinga Wametoa kauli hiyo katika mkutano mkuu wa Mwaka wa Chama Hicho na kwamba vyama vingi vya msingi vinaingia Migogoro kutokana na kushindwa kushughulikiwa kwa baadhi ya Changamoto ambazo Zinawarudisha nyuma.
Mwenyekiti wa Chama kikuu Cha ushirika mkoa wa Njombe NJORECU Stephano Luoga na Mjumbe wa bodi wa Chama hicho Yohana Mhagama wamesema jitihada mbalimbali zimeshachukuliwa na wanaendelea kutatua changamoto hizo kwa maslahi Mapana ya ushirika.
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Njombe Edmund Masawe amewataka wanachama na vyama vyao kutunza kumbukumbu ili ziweze kuwasaidia katika kutatua Migogoro ya mali za ushirika.
Wadau wa pembejeo za Kilimo akiwemo Dokta Mshindo Msola Bwana shamba Toka Kampuni ya minjingu anawataka wakulima kuendelea kutumia mbolea zinazopatikana katika maghala yao yaliyokaribu wakati wakiangalia uwezekano wa kufungua viwanda katika mikoa ya Kusini mwa Tanzania.
0 Comments