Header Ads Widget

MAAFISA UTUMISHI NA WASIMAMIZI WA SHERIA KUONGEZA UWAJIBIKAJI


.NA CHAUSIKU SAID 
MATUKIO DAIMA 

Serikali kupitia Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala imewataka maafisa utumishi na wasimamizi wa Sheria kuongeza uwajibikaji katika nafasi zao ili kupunguza malalamiko ya watumishi Kwa viongozi wa juu.

Hayo yamebainishwa Leo Jijini Mwanza na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Deus Sangu katika kikao kazi kilichowakutanisha maafisa utumishi na wasimamizi wa sheria juu ya kutatua changamoto za utekelezaji wa Sheria ya Utumishi wa Umma na kanuni zake.

Ameeleza kuwa wamekuwa wakipokea barua nyingi za ufafaunuzi wa maswala mbalimbali ya kiutumishi ambayo tayari yamekwisha kutolewa ufafunuzi wa maelekezo hivyo kupelekea mambo hayo kuonesha ni moja ya sababu ya watu kutowajibika ipasavyo katika kusimamia sera, kanuni, taratibu na Sheria zilizowekwa.

"Tumekuwa tukiletewa Kila siku ofisini barua za kupandishwa vyeo mambo ambayo yanapaswa kufanya na afisa utumishi lakini hawafanyi hiyo mpaka mtu anaamua kwenda ofisini za utumishi kutokana na watu kutowajibika Kwa ufasaha katika  kazi zao ipasavyo" Alisema Sangu.

Aidha Kwa upande mwingine ameeleza kuwa Kuna jambo la rushwa limeibuka Kwa mtumishi wa umma ili mtu asaidiwe ni lazima atoe rushwa huku akieleza kitendo hicho ni kunyume na mabadiliko ya kazi na kuwataka wahakikishe wanatenda haki na kuachana na vitendo vya rushwa kwani inafubasha maendeleo ya taifa na kusababisha maendeleo ya Nchi kurudi nyuma.

Kaimu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Silas Kapinga ameeleza kuwa kumekuwa na kasumba kutoka Kwa watumishi kutofata Sheria, kanuni na miongozo ya kazi. 

" Katika utekelezaji meseji imeonekana haifiki Kwa usahihi ndio maana tumeamua kutumia mfumo wa kikanda ili kupata uwakilishi Mpana ili meseji ifike Kwa upana na Kwa wakati ili kutatua changamoto zinazotukabili" Alisema Kapinga

 Kwa upande wake Mkurugenzi Huduma za haki na Sheria kutoka Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Hilda Kabisa amesema kuwa Kuna changamoto mbalimbali wanakutana nazo katika utekelezaji wa Sheria, kanuni na taratibu katika kusimamia rasilimali watu.




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI