Header Ads Widget

UJUMBE WA RC MTAMBI KWA VIONGOZI WA DINI KWENYE TUKIO LA IFTAR KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

 


Na Shomari Binda-Musoma 

VIONGOZI wa dini wameombwa kusaidia serikali katika mapambano ya kuzuia ukatili na mmomonyoko wa maadili na kujiepusha na kauli tata kuelekea uchaguzi mkuu.

Mapambano ya viongozi hao ni kuelekezwa kwenye maombi na kuzungumza na waumini kwenye nyumba za ibada Misikiti na Makanisa.

Ujumbe huo umetolewa jana machi 27 2025 na mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Mtambi wakati wa tukio la Iftar lililofanyika Ikulu ndogo ya Mkoa wa Mara.

Amesema viongozi hao ni sehemu ya kukemea mmomonyoko huo wa maadili kwenye jamii na watu ama kundi linalojaribu kupotosha dhidi ya utulivu uliopo nchini.




Mtambi amesema viongozi hao kupitia mimbali na mazabahu wanasikilizwa na waumini hivyo ni rahisi kupokea na kusimama kwenye mstari.

“Niwaombe sana viongozi wa Dini tusaidieni katika hili kwenye maeneo yenu hasa ya ibada tuanahitaji kila moja kuwa mlinzi wa Iman yetu nakuhakikisha hadi hapa alipotufikisha Dkt. Samia Suluhu Hassan tunapalinda.

"Suala la mmomonyoko wa maadili lipo kwenye jamii zetu na nyie mnao uwezo mkubwa wa kusaidiana na serikali kuikumbusha jamii na ikawasikiliza",amesema.

Katika hatua nyingine RC Mtambi amesema serikali itashirikiana na viongozi hao katika kuunganisha nguvu katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo



Sheikh wa mkoa wa Mara Msabaha Kassim amesema wataendelea kushirikiana na serikali kama ujumbe ulivyotolewa na mkuj huyo wa mkoa ili jamii isimame kwenye maadili na kuwa na hofu na Mungu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Malidhiano ya Viongozi wa Dini mkoani Mara Askofu Rutubija Rutubija amesema  suala maadili mema yana mchango mkubwa kwenye jamii na wanakwenda kuyasimamia ili kuwa na jamii bora.

MWISHO.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI