Na Shomari Binda-Musoma
KAMPENI Maalum iliyopewa jina la"Mkomboe Nyangeta na Athumani Kielimu" Musoma Vijijini imezinduliwa rasmi jana machi 27,2025. Jimbo la Musoma Vijijini.
Mkuu wa Wilaya ya Musoma Juma Chikoka amezindua kampeni hiyo baada ya kufanyika mjadala wa siku 3 wenye lengo la uboreshaji,ufundishaji na uelewa wa wanafunzi uliowashirikisha walimu,waratinu wa elimu,watendaji wa vijiji,madiwani na wadau mbalimbali.
Akizungumza na washiriki wa mjadala huo uliokuja na mapendekezo 16 yenye lengo la kuinua kiwango cha elimu na ufaulu mkuu huyo Wilaya amesema moja ya pendekezo ni kampeni hiyo na kutaka ianze mara moja.
Amesema kampeni hiyo itaendana na suala la chakula kwa wanafunzi kuwa cha lazima kwa wanafunzi wanapokuwa shuleni na kuwataka watendaji wa vijiji kuanza utekelezaji wake kwa kuwashirikisha wazazi na walezi wa wanafunzi.
Chikoka amesema mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amekuja na maono makubwa ya kuleta mjadala huo kwa kuwaleta waadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Dar es sala ( UDSM) kwa gharama zake ili kuongoza mjadala huo hivyo lazima matokeo yaonekane.
" Ngugu katika kufanikisha lengo la mjadala huu wa siku 3 na mapendekezo yaliyokuja natangaza kuzindua kampeni ya "Mkomboe Nyangeta na Athumani Kielimu" ianze mara moja.
" Yote yaliyo kwenye mapendekezo tutakwenda kuyafanyia kazi na kila mmoja atekeleze majukumu yake katika kufanikisha kupandisha kiwango cha elimu na ufaulu jimbo la Musoma Vijijini"amesema.
Aidha mkuu huyo wa Wilaya amezindua tuzo za kila mwaka za walimu na shule zinazofanya vizuri kwenye matokeo,utoaji wa chakula kwa wanafunzi na utunzaji wa mazingira ambapo waliofanya vizuri kwa mwaka 2024 wamepewa vyeti na zawadi ya frdha taslimu.
Kwa upande wake mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema kipaumbele ndani ya jimbo ni suala la elimu na ndio kusudio la kuleta mjadala huo pamoja na kuanzishwa kwa utoaji tuzo.
Amesema kila mmoja akitimiza majukumu yake suala la wanafunzi kupata ziro kwenye jimbo la Musoma vijijini itakuwa historia.
Awali akiwasirisha mapendekezo ya mjadala huo mmoja wa wakufunzi hao Dk.George Kahangwa amesema alichokifanya Profesa Sospeter Muhongo kina maana kubwa na kitaleta mageuzi makubwa kielimu na kusisitiza kila mmoja kuwajibika
Walimu,waratibu elimu Kata watendaji wa vijiji,madiwani na wadau wa elimu walioshiriki mjadala huo kwa nyakati tofauti wamesema wanakwenda kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na kile walichojifunza ili kuweza kufikiwa kwa malengo tarajiwa.
Ame
0 Comments