Header Ads Widget

SERIKALI YAVUNA SH BILIONI 3 NDANI YA MIEZI 8 KUPITIA SEKTA YA MADINI KAGERA

🔴*Serikali yavuna Shilingi Bilioni 3 ndani ya miezi 8*

🟤· *Ni kupitia Sekta ya Madini Kagera*

🟤· *Waita wawekezaji ndani na nje*

MAKUSANYO ya maduhuli ya Serikali kupitia Sekta ya Madini katika Mkoa wa Kagera yatokanayo na mrabaha, tozo na ada mbalimbali kwa mwaka wa fedha  ulioanza Julai 2024/ 2025 ni Shilingi Bilioni 3.2

Kagera ilipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 5.8 na mpaka mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu wa 2025 wamefanikiwa kukusanya kiasi hicho cha fedha kikiwa ni sawa na asilimia 82 ya lengo katika kipindi cha miezi nane.

Akizungumza Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kagera, Nobert Mkopi amesema fedha hizo zimekusanywa kutokana na  jitihada mbalimbali walizofanya katika usimamizi wa Sekta ya Madini katika halmashauri  zote saba za Mkoa wa Kagera.

“Mkoa wa Kagera kwa maana Sekta ya  Madini tunasimamia  halmashauri zote saba kwa maana ya wilaya za Kyerwa, Karagwe, Misenyi, Muleba, Bukoba, Biharamulo na Ngara, kuna shughuli mbalimbali  za uchimbaji madini,”amesema  Mkopi na kuongeza,

“Mkoa huu yanapatikana madini mbalimbali ikiwemo Bati, Dhahabu, Nickel, Wolframite (WO3), Madini ya Viwandani na  Madini Ujenzi.

“Maeneo ya Kyerwa yanachimbwa madini ya bati, yanachimbwa kihalali kwa leseni za uchimbaji mdogo lakini pia kuna leseni kubwa ya utafiti na madini haya yanachangia asilimia 32 mpaka sasa ya maduhuli tuliyokusanya ya Shilingi Bilioni 3.2 na fedha nyingine zinatoka kwenye madini mengine ikiwemo dhahabu na ada mbalimbali za vibali na leseni" amesema Mkopi

Aidha amesema  mwenendo wa ukusanyaji maduhuli  sio mbaya  na   hadi kufikia mwisho wa mwaka wa fedha wana imani  watafikia lengo lililokusudiwa.

Katika hatua nyingine, Mkopi ametoa wito kwa wawekezaji kote nchini kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika Sekta ya Madini mkoani Kagera ambao una utajiri mkubwa wa madini mbalimbali ikiwemo Bati, Dhahabu, Nickel, Wolframite (WO3), Madini ya Viwandani na  Madini ujenzi.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI