Na Costantine Mathias, Bariadi,
MKUU wa Mkoa wa Simiyu Kenan Kihongosi leo 04 Machi, 2025 ameongoza kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Simiyu katika ukumbi wa mikutano wa Bariadi.
Akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho, Kihongosi amewapongeza Wakala wa Barababara Nchini TANROADS pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA kwa kazi nzuri wanayofanya ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Amewasisitiza Wakala wa Barabara Nchini TANROADS pamoja na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini TARURA, kuhakikisha wanalipa madeni ya wakandarasi wanaotekeleza miradi ya barabara ili kuharakisha ukamilikaji wa miradi kwa wakati.
Aidha amewataka kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa Mkoani Simiyu inalingana na thamani ya Fedha.
Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani Simiyu hufanyika mara mbili kwa Mwaka kutathmini utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Barabara.
Mwisho.
0 Comments