Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya sita inaendelea na mikakati mbalimbali ya kuhakikisha Mikoa ya kaskazini mwa Tanzania inaondokana na changamoto ya kukatika kwa umeme mara kwa mara ambapo imeanza mazungumzo na nchi jirani ili kununua umeme katika kuhakikisha mikoa hiyo inakuwa na utoshelevu wa Umeme.
Hatua hiyo kulingana na Rais Samia aliyekuwa akizungumza na wananchi wa Same katika uzinduzi wa mradi wa maji wa Same-Mwanga-Korogwe leo Machi 09, 2025, Rais Samia amesema zoezi hilo linaenda sambamba na maboresho makubwa ya sekta ya maji katika kuhakikisha kuwa Wilaya za Same na Mwanga zinakuwa na Maji safi, salama na ya uhakika.
Hatua ya ununuzi wa umeme kutoka nje ya nchi unatokana na kilio cha muda mrefu cha wakazi wa Mikoa ya Arusha na Kilimanjaro, ambao wamekuwa wakiathirika na kukatika kwa umeme mara kwa mara, suala ambalo limekuwa likirudisha nyuma shughuli mbalimbali za uzalishaji kwenye Mikoa hiyo.
0 Comments