Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI MHE.SANGU : UTASHI WA KISIASA WA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN UMEIWEZESHA TAKUKURU KUWAJIBIKA

Na.Mwandishi wetu- Kilimanjaro

 Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deus  Sangu amesema utashi wa kisiasa wa Rais  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan umeiwezesha  TAKUKURU kupata vitendea kazi na kutimiza majukumu yake kwenye mazingira wezeshi.

Amesema katika kipindi cha Serikali ya Awamu ya Sita zaidi ya Watumishi 1000 wameajiriwa na TAKUKURU, ikiwa ni jitihada  za Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuiwezesha TAKUKURU.

Mhe.Sangu ametoa kauli hiyo wakati Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria ilipotembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la  TAKUKURU,  Wilaya ya Rombo, Mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni muendelezo wa ziara ya  Kamati hiyo kukagua  miradi mbalimbali iliyotekelezwa na   Taasisi zilizo chini ya Ofisi ya Rais, UTUMISHI na Utawala Bora.

Amesema mbali na magari 88 TAKUKURU iliyowezeshwa, inatarajia kwa mara nyingine tena  kupokea jumla magari 100 ili kuwasaidia  maafisa hao kutekeleza majukumu yao mahali popote na saa yeyote wanakohitajika.

Amesema hiyo ni nia ya dhati ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha  TAKUKURU inakuwa na vitendea kazi vya kutosha na vya kisasa.

"Taasisi yetu sio tu inaziangalia Taasisi nyingine bali imekuwa mfano na kioo kwa Taasisi nyingine katika kuonesha thamani halisi ya fedha iliyotumika katika ujenzi wa jengo hili la Rombo" Mhe. Sangu amefafanua.

Katika hatua nyingine Mhe.Sangu ametoa  pongezi kwa Kamati hiyo  kwani ndiyo imekuwa ikifanya  mambo yatokee, " mmekuwa mkipaza sauti kwa  kufanya mapendekezo ya marekebisho ya bajeti kwenye miradi ya maendeleo kwenye Taasisi yetu ya TAKUKURU" 

Amefafanua kuwa mwaka jana bajeti ya TAKUKURU ilikuwa Sh. Bilion 4.5 ambayo Kamati hiyo iliwatupigania na mwaka huu wa fedha imekuwa Sh. Bil. 6, "Bila kelele ya Kamati yako Mhe.Mwenyekiti tusingepata fedha hizi" amesisitiza




 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI