Header Ads Widget

MWENYEKITI WA CCM KATA YA KAMNYONGE AMSHUKURU MBUNGE MATHAYO UTEKELEZAJI WA AHADI YA VITI

Na Shomari Binda-Musoma Matukio                                    Daima App 

MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi ( CCM) Kata ya Kamnyonge Emanuel Bwimbo amemshukuru mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo kwa kutekeleza ahadi yake ya kuwapa viti 50.

Ahadi hiyo imetekelezwa leo machi 8/2025 na Katibu wa mbunge huyo Christopher Majala kwenye ofisi za chama hicho Kata ya Kamnyonge.

Akipokea viti hivyo Mwenyekiti huyo amesema kutokana na upungufu wa viti kwenye ofisi yao walifikisha ombi kwa mbunge machi 3/2025 alipofanya ziara ya kuitembelea Kata hiyo na kwa muda mfupi ameitekeleza.

Amesema licha ya maombi ya viti ambavyo tayari wamevipata walitoa maombi ya kukarabatiwa kwa jengo la ukumbi ambao pia ameahidi kuanza ukarabati wake hivi karibuni.

Bwimbo amesema ilikuwa ikiwapelekea kukodisha viti wanapotaka kufanya vikao lakini kwa sasa adha hiyo itakuwa haipo kutokana na mbunge kuwashika mkono.

" Tunamshukuru sana mheshimiwa mbunge Mathayo kwa leo kutekeleza ahadi yake ya viti baada ya kufikisha maombi kwake.

" Ni juzi alitutembelea hapa na kumfikishia maombi yetu lakini leo katibu wa mbunge ametuletea viti tunamshukuru sana mbunge na tuko pamoja nae",amesema.

Licha ya Kata hiyo ya Kamnyonge alipokuwa kwenye ziara yake ya Kata kwa Kata hivi karibuni mbunge wa jimbo la Musoma mjini Vedastus Mathayo alipokea maombi ya viti kutoka Kata za Nyamatare,Iringo pamoja na Nyasho ambao pia wamekabidhiwa viti hii leo.

Akikabidhi viti 100 kwa Kata hizo,Katibu wa mbunge Cristopher Majala amesema mbunge anatekeleza ahadi zake za maombi mbalimbali aliyoyapokea kutoka kwa viongozi wa chama ngazi ya Kata wakati wa ziara yake.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI