Header Ads Widget

MFANYABIASHARA RAMA MSOMI AONGOZA WAUMINI WA DINI YA KIISLAM KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI

Na Shomari Binda-Musoma Matukio Daima 

MFANYABIASHARA Ramadhan Msomi ameongoza waumini wa dini ya Kiislam kuchangia ujenzi wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa mjini Musoma.

Mara baada ya swala ya ijumaa na mawaidha yaliyotolewa na mlinganiaji wa dini ya Kiislam na Naibu Katibu Mkuu wa Waadhiri wa Kiislam Tanzania Sheikh Muhamed Lwambo mfanyabiashara huyo alichangia kiasi cha shilingi milioni 1 na kukusanywa jumla ya shilingi milioni 4 na laki 7.

Akizungumza Msikitini hapo Sheikh Lwambo amewashukuru waumini wa dini ya Kìslam mkoani Mara kwa Jihad yao ya ujenzi wa Msikiti kwa michango yao

Amesema Msikiti wa kisasa unaojengwa mkoani Mara kupitia michanho ya waumini ni mfano wa kuigwa na maeneo mengine.

Sheikh Lwambo amesema misikiti mikubwa kama hiyo mara nyingi inajengwa na wafadhili hususani kutoka nchi za kiarabu na mataifa makubwa.

Amesema watu wa Musoma na mkoa wa Mara waliopo ndani na nje ya mkoa wamekuwa mstari wa mbele kuchangia hata kwa kupigiwa simu.

" Tupo katika kumi la mwisho la mwezi mtukufu wa Ramadhan na hakuna swadaka kubwa kama ujenzi wa Msikiti kama mnavyofanya hapa.

" Mnafanya jambo kubwa katika dini na mtaraji malipo mskubwa hapa duniani na kesho akhera kwa jitihada kubwa mnayoifanya",amesema.

Sheikh wa mkoa wa Mara Msabaha Kasim amemshukuru Sheikh Lwambo kutoka Dar es salam kwa kufika Msikitini hapo na kuzungumza na waumini katika umuhimu wa swadaka ya ujenzi wa Msikiti.

Amesema bado wanawakaribisha na kuwapokea wageni kutoka maeneo mbalimbali ili kuweza kuzungumza na waumini na kuchangia ukamilishwaji wa Msikiti huo.


 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI