WANAWAKE 400 WATEMBELEA ENEO LA HIFADHI YA NGORONGORO NA KUSHUHUDIA "BIG FIVE
Akizungumza na wanawake hao baada ya kuwapokea leo tarehe 7 machi, 2025 Kamishina Msaidizi Mwandamizi anayesimamia idara huduma za Utalii na Masoko, Mariam Kobelo amesema ujio wa wanawake hao utaendelea kuhamasisha utalii wa ndani kwenye vivutio vilivyopo ndani ya hifadhi hiyo.
Wanawake wa jamii ya Kihadzabe wapaza sauti siku ya wanawake duniani "Tukiwa tunaelekea kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani, Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) tunatumia fursa hii kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo ndani ya Eneo la Hifadhi, na Leo kwa kushirikiana na Kampuni ya Utalii ya Tanzanite Cooperates tumepokea wanawake takriban 400 waliokuja kutalii". Alisema Mariam.
Aidha, Mariam alisisitiza kuwa NCAA imejiandaa vyema kuhakikisha kuwa ziara hiyo ya kitalii itatumika kuleta chachu kwa watanzania wengine ikiwa ni jitihada za Kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Naye, Mkurugenzi wa Kampuni ya kitalii ya Tanzanite Cooperates, Bi. Elina Mwangomo alisema kwamba Kampuni yake imejikita zaidi kwenye utalii wa ndani na imekuwa ikifanya ziara za kutembelea Hifadhi mbalimbali nchini ambapo bonde la kreta limekuwa sehemu pekee ambapo watalii wanaweza kujionea wanyama wengi kwa karibu zaidi ndani ya muda mfupi.
" Kreta ya Ngorongoro ni sehemu pekee ambako watalii wetu wengi wamekuwa wakivutiwa kuja kutembelea na kwa muda sasa tumekuwa tukija na makundi mbalimbali na Leo tuko na kundi la takriban wanawake 400 ambao tumekuja kutalii na kufurahi pamoja tukielekea kilele cha maadhimisho ya siku ya Wanawake duniani" Alisema
Elina
Kwa upande wake Bi.Gloria Mziray kutoka Mfuko wa taifa wa bima ya Afya (NHIF) Arusha ambaye ni mmoja kati ya wanawake waliokuwa kwenye ziara hiyo alieleza kuwa safari yao ndani ya Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro imekuwa ya kipekee sana na wamefurahishwa kuona wanyama mbalimbali waliopamba hifadhi hiyo wakiwa kwenye Mazingira yao ya Asili.
Bi. Fatuma Abduli kutoka benki ya CRDB ambao wamekuwa wadau wakubwa wa utalii nchini pamoja na kufurahishwa na upekee wa Kreta ametoa wito kwa watanzania kujenga hulka ya kutembea vivutio mbalimbali vilivyopo ndani ya nchi.
Wakiwa katika hifadhi hiyo wanawake hao pamoja na watalii wengine waliotembelea maeneo ka Kreta ya Ngorongoro na tambarare za Ndutu wameshuhudia vivutio mbalimbali ikiwemo wanyama wakubwa maarufu kama "Big Five" ambao ni Faru, Tembo, chui, Nyati na Simba
Kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yatafanyika Machi 08, 2025 Mkoani Arusha ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
NA: Maipac Team- Eyasi
Wanawake wa Jamii ya wahadzabe wanaoishi katika eneo la Eyasi wilayani Karatu Mkoani Arusha wamepaza sauti katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kumuomba Rais Samia Suluhu asikilize kilio chao.
Wakizungumza katika mdalaho wa siku ya wanawake, uliofanyika katika Kijiji cha Qandet eneo la Eyasi wilaya ya Karatu, kwa kuandaliwa na taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) kwa kushirikiana na Kituo cha Radio cha SAVVY FM, Wanawake hao, wameeleza wanakabiliwa na changamoto lukuki.
Katibu wa Wahadzabe eneo la Eyasi, Maria Yona anasema wanamuomba Rais Samia kuwasaidia wapate ardhi, maji, chakula na kuzuia uvamizi wa ardhi yao.
“Tunatamani sana kumuona Rais Samia Mwanamke mwenzetu, tumweleze sisi wanawake wa Kihadzabe tunaishi katika maisha magumu sana, hatuna maji, hatuna ardhi na chakula”anasema
Anasema ardhi yao ya asili inaendelea kuvamiwa na wakulima na kusababisha kukosa hadi chakula cha asili, ikiwepo matunda, mizizi na asali.
Maria anasema, wanawake wa jamii ya Kihadzabe ni masikini sana na hawajawahi kufikiwa hata na mikopo midogo midogo ya halmashauri kama walivyo wanawake wengine.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahadzabe, Mdindi Samboga anasema wanawake na wanajamii wengine wa kihadzabe, wanaiomba serikali kuwamilikisha ardhi yao kama ilivyo jamii nyingine.
“Wahadzabe wenzetu wa yaeda chini, wilaya ya Mbulu wamepata hati miliki ya kimila za maeneo yao hivyo hawavamiwi sana na sisi tunaomba kusaidiwa” anasema
Mhadzabe mwingine, Ng’o Nkoo anasema hawajuwi maana ya maadhimisho ya siku ya wanawake, kwani wao hawajawahi kushiriki lakini kubwa maisha yao yamekuwa ya shida sana.
“hatuna ardhi, hatuna chakula, vijana wanashindwa kuoa kwa sababu hakuna Wanyama na asali ya kupeleka mahari na Chanzo cha haya ni ardhi yetu ya asili kuendelea kuvamiwa”anasema
Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Baray, Kassim Miraji anakiri kuwa wanawake wa jamii ya kihadzabe bado hawajafikiwa na mikopo na kutokana na maombi yao, watafanyia kazi suala hilo.
“Serikali ya Rais Samia Suluhu imetoa fedha za mikopo kwa wanawake na katika eneo hili mimi ndio napaswa kushughulikia ninaahadi kuanzia leo ntaanza kuwasaidia kujiunga katika vikundi ili wanufaike na mikopo”anasema
Mwenyekiti wa bodi ya Utalii katika eneo la Lake Eyasi, Daniel Hhawu anasema ni kweli jamii ya Kihadzabe wakiwepo wanawake wanakabiliwa na shida nyingi licha ya kuwa kivutio cha watalii.
“Ni kweli ardhi yao inavamiwa na wanakosa chakula ila mambo haya yapo chini ya serikali sisi kama bodi ya Utalii katika eneo hili hatuhusiki na masuala ya ardhi na kilio chetu tunaomba wasaidiwe”anasema
Mkurugenzi wa MAIPAC, Mussa Juma anasema wameamua kuifikia jamii ya Wahadzabe ili kujua changamoto za jamii hiyo hasa wanawake na Watoto.
“Wameeleza shida ya ardhi yao kuvamiwa, wameeleza kukosa maji, chakula cha asili na huduma nyingine muhimu lakini pia tumehamasisha wajitokeze kushiriki katika uchaguzi mkuu, kwa kugombea nafasi mbali mbali”anasema
Kaimu Meneja wa SAVVY FM, Neema Twazihirwa akizungumza katika mdahalo huo, anasema radio yao kwa kushirikiana na MAIPAC wataendelea kushirikiana na jamii ya Wahadzabe kupaza sauti zao juu ya kero zinazowakabili.
Twazihirwa anasema wao kama wanahabari, wataaandaa vipindi maalum ambavyo vitasaidia kupaza sauti za jamii hiyo, ili waweze kupata misaada mbali mbali.
Katika Maadhimisho hayo, MAIPAC na SAVVY FM pia walitoa msaada wa vitu mbali mbali kwa wanawake wa jamii ya Kihadzabe na Watoto.
Katika kuelekea maadhimisho ya kitaifa ya siku ya wanawake Duniani, MAIPAC na SAVVY FM kwa msaada wa wadau mbali mbali ikiwepo wafanyakazi wa UN Women imewasafirisha wanawake wa jamii hiyo, kuhudhuria sherehe za kitaifa jijini Arusha, Leo Machi 8, katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid ambapo mgeni rasmi atakuwa Rais Samia Suluhu Hassan.
MWISHO.
Mbinu ya kupata maendeleo ya kifedha katika ndoa
Naitwa Mama James, nimeolewa na mwanaume mwenye watoto wawili ila kila mtoto ana mama yake pia wanaishi na mama zao sipo nao, na mimi nimemzalia watoto wawili pia, kwa hiyo kwa jumla ana watoto wanne.
Huyu mkubwa kamaliza kidato cha nne mwaka 2021 ila kafeli mwingine kaanza kidato cha kwanza mwaka huu sasa vifaa vya huyo mtoto vilichukua zaidi ya Sh300,000 na mume wangu hana kipato kivile.
Hapa ndani ilikuwa ili kupata fedha ni hadi nijibane tena kwa tucheze mchezo ndo tuendeshe mambo, kwa hiyo mchezo uloisha ndio tuliomlipia huyo mtoto wa kidato cha kwanza mahitaji yake ya shule.
Tulivyoanza mchezo tena, sasa akawa ananiambia mama anaumwa kila siku mara katuma elf 30 mara 50, mara anarudi hospital kesho inatumwa 40, yaan mpaka nikawa nachoka maana mambo yote tulisimamisha ili tumtoe huyu wa kidato cha kwanza.
Baada ya hapo tulipokea mchezo ili tuendeleze ujenzi tununue tofali kidogo kidogo, ila mambo nayo yakaingiliana kila siku ni kutuma hela. Siongei kwa ubaya ila nalihisi kukata tamaa kabisa.
Nikawa najisema yaani hivi kuolewa na mwanaume mwenye watoto ndio hatari hivi na haswa awe ndio tegemezi nyumbani kwao yaani hakuna maendeleo kabisa ambayo mnaweza kufanya.
Nalivyokuwa najibana sikumbuki mara ya mwisho kununua nguo ilikuwa lini hela zote kwenye mchezo na mchezo ukipatikana majukumu ya wanae na ndugu zake kama yote.
Na nilivyokuwa napambana ili tujenge nilijua ile nyumba sio yangu na wanangu tu bali hata hao watoto wengine inawahusu sasa nilihisi kukata tamaa kabisa nikataka nianze namna ya kuponda raha tukipokea mchezo niwe naingia tu dukani nisije tembea uchi.
Wakati nikiwa na mawazo hayo, nikasikia kuwa Kiwanga Doctors wanaweza kukusaidia kupata kazi, ndipo nikachukua hatua ya kuwasiliana naye ili nami nipate hata kazi ya maana niweze kuwa na maisha mazuri maana mume kashindwa kunipa.
Mtaalamu huyo anayepatikana huko Migori nchini Kenya, akanifanyia matambiko yake ya kupata kazi (job spells) na kweli nikaja kupata kazi na sasa nimemsaidia na mume wangu kumalizia ujenzi na nina maisha mazuri tu.
Kwa hakika sitochoka kumshukuru Kiwanga Doctors kwa jinsi ambavyo amenisaidia kuinua kipato changu. Basi wasiliana naye kwa namba +254 116 469840 au tembelea tovuti yao.
0 Comments