Hivi Amos Makala amesema anachokijua au anajua alichokisema!?
Katibu Mwenezi wa CCM, Amos Makala ameongea kwenye mkutano wake wa hadhara na kuwaeleza umma wa watanzania kuwa "Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimepanga kutumia virusi vya Ebola na M pox kuzuia uchaguzi mkuu usifanyike mwaka huu 2025." Makala.
Lakini Chadema tangu wametangaza msimamo wao wa No "Reforms No Election", wamekuwa wakitoa ufafanuzi wa maneno hayo, pengine kosa lao ni kutumia lugha ya kigeni ya waingereza kuwaeleza waswahili.
Hili la lugha, ni sawa naweza kukubaliana na wote wanaohitaji tafsiri au ufafanuzi kwa kuwa inafahamika wazi kuwa watanzania wengi hawajui kimombo, si wale tu wasiosoma bali hata wanaojiita wasomi nao hawakijui kiingereza.
Mara kadhaa viongozi wengi wa CCM, hata msajili wa vyama vya siasa naye alitoa wito kwa viongozi wa Chadema kwamba waende ofisini kutoa ufafanuzi wa maneno haya ya 'No reforms no election.'
Kitendo cha katibu mwenezi wa CCM, Amos Makala kutoelewa maana ya maneno hayo kiasi kwamba ameyatafsiri kuwa yanamaanisha Chadema kuwa na mpango wa kuleta virusi vya Ebola na M pox, ni kielelezo cha elimu yetu ilivyo haitoi uelewa kwa raia wa nchi hii.
Mimi siamini kama Makala ni mjinga kiasi hicho, labda kwa kajitoa ufahamu makusudi kwa kuwa pengine anajua watanzania wengi hawajasoma hasa ktk kuijua lugha ya kiingereza.
Kama ndivyo basi hakujua anachokisema, na badala yake amesema anachokijua yeye.
Ni hatari sana kwa kiongozi asiyekuwa makini na anachokiongea kwa watu anaowaongoza, ukiwa kiongozi lazima ujue unachokiongea.
Makala amesema Chadema wamejipanga kuleta virusi vya Ebola na M pox kuzuia uchaguzi mkuu, kwa akili na mtazamo wake aliamini taarifa hizi zitawafanya wananchi waichukie Chadema kwa kuwaletea magonjwa hatari ya virusi vya Ebola na M pox ili wafe.
Kuna methali inasema "Haidhuru hudhuru", mtu ye yote anayeona dalili za kuharibika kwa jambo, halafu akasema " haidhuru" baadaye linaweza kuwa na matokeo mabaya ambayo yatamdhuru mtu au watu.
Uongo ni sumu mbaya inayoathiri wanaoongopewa na anayewaongopea.
Ambacho hakukijua Katibu Mwenezi wa CCM, Amos Makala, ni kwamba ameuambia umma wa watanzania na duniani kote kuwa magonjwa kama haya ya kigeni na hatari zaidi, kumbe yanaweza kusafirishwa na kwenda kumwagwa mahala au nchi fulani kwa lengo maalumu fulani la kuwadhuru wanadamu.
Na kwamba magonjwa haya hutengenezwa na watu wenye nia ovu kwa madhumuni fulani la kuua binadamu, likiwemo la kibiashara kama ilivyo kwa UKIMWI na Korona.
Hichi ndicho kilichopo DR Congo ambako wazungu wanachimba madini.
Na kusema kweli Makala asipotengua kauli yake hii, itaifanya CCM ichukiwe zaidi na wananchi kuliko matarajio yake kwamba wananchi waichukie Chadema.
CCM tuleteeni Paul Makonda viatu vyake alivyoviacha vimeshindikana kuvaliwa na Makala, ni vikubwa mno.
Kwiyeya Singu. 0784977072
0 Comments