Moja ya jengo la zahanati kata ya kishiri Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza
Mwakilishi wa Mratibu Tasaf James Hutler akitoa taarifa fupi juu ya Miradi inayotekelezwa na Tasaf Wilaya ya Nyamagana
Mwenyekiti wa kamati ya usalama ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akitoa ufafanuzi Kwa baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama
NA CHAUSIKU SAID
MATUKIO DAIMA
Kamati ya usalama Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza imewataka wasimamizi wa Miradi ya ujenzi inayotekelezwa na Tasaf kubadilisha miundombinu iliyowekwa katika Miradi mbalimbali ambayo haiendani na viwango vinavyohitajika.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa usalama Wilaya ya Nyamagana ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya Amina Makilagi katika ziara ya kutembea Miradi mbalimbali inayotekelezwa na Tasaf na kueleza kuwa wametembelea Miradi Touti tofauti na kukuta baadhi ya Miradi ahijakizi viwango.
Makilagi ameeleza kuwa watalaamu wanapaswa kujenga na kuweka miundombinu Kwa kuzingatia viwango vinavyokubalika ili kupata matokeo chanya ya fedha zinazoletwa Kwa wananchi, pia miradi yote ya Tasaf inayoendelea Jiji la Mwanza kuhakikisha inazingatia ubora Kwa Kila kitu kuanzia kumpata fundi, ujenzi na umaliziaji wa majengo ili Miradi iweze kuleta matokeo yanayostahili.
"Mfano tumekwenda baadhi ya Miradi tumekutana na mbao ambazo hazikubaliki kama seplasi ziondolewee na maeneo mengine tumekutana na mirango ya mitundu na ni marufuki kuweka mirango ya mitundu kuweka katika Miradi yetu ya maendeleo"Amesema Makilagi.
Aidha ameeleza kuwa ambao hizo wanazotumia huliwa na wadudu, haistahimili wakati wa joto na baridi hulepekea kuvimba na kusababisha milango hiyo kutofunga jambo ambali linaweza kuonesha tumejenga Miradi chini ya kiwango
"Tumieni mbao zinazokubalika na kumekuwa na tabia ya watu kubeba mbao zozote na kushindwa kuleta mbao ambazo zinazostahili na wale mnaosimamia mkiwemo CMC na zile kamati mnazopokea vifaa kabla ya kupokea vifaa vikague mjilizishe ndio vipokelewe" Alisema Makilagi.
James Hutler Mwakilishi wa Mratibu Tasaf ameeleza kuwa Miradi wanayotekeleza ni Elimu, Afya pamoja na miundombinu ya barabara ambapo jumla yake ni 17 ambayo imegahrimu kiasi Cha Sh Bil 267 ambapo mwishoni mwa mwezi huu Miradi 15 itakabidhiwa.
Abed Munda na Lucia Deus wasimamizi wa maendeleo ngazi ya jamii (CMC) wameeleza kuwa changamoto wanazokutana nazo katika usimamizi wa ujenzi kutopata vifaa Kwa wakati na vingine kuletwa nusunusu na kupelekea mafundi kufika katika eneo la kazi na kukaa pamoja na ucheleweahaji wa posho Kwa wasimamizi wa Miradi.
Mtendaji wa kata ya kishiri John Mwakilosa ameipongeza serikali kujenga zahanati itawasaidia wananchi kupata matibabu Kwa wakati, pia Kwa upande mwingine ameomba kupatiwa uzio utakaowasidia kulinda mipaka ya zahanati.
Aidha Kwa upande wake mwenyekiti wa mtaa ya mash road Petro Yanonaga ameiomba serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuwakamilishia mradi wa barabara ya mawe ya mash road ili iweze kupitika Kwa urahisi kutokana na kufungwa Kwa muda mrefu.
0 Comments