Header Ads Widget

BODABODA, BAJAJI WAPEWA NENO UJENZI BARABARA ZA LAMI NCHINI

 

Askari wa kikosi cha usalama barabarani Wilaya ya Kasulu Emanuel Fusi akizungumza katika mkutano wa kutoa elimu kwa waendeshaji vyombo vya moto uliofanyika kituo kikuu cha mabasi wilayani Kasulu


Mkuu wa kituo cha kikanda cha  umahiri wa usalama barabarani Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, Godlisten Msumanje akizungumza katika mkutano wa utoaji elimu kwa madereva wa vyombo vya moto kwenye stand kuu ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Mkuu wa kituo cha kikanda cha  umahiri wa usalama barabarani Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, Godlisten Msumanje akizungumza katika mkutano wa utoaji elimu kwa madereva wa vyombo vya moto kwenye stand kuu ya wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma

Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Kituo cha umahiri wa usalama barabarani Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika kimewataka watumia vyombo vya moto barabarani kuwa na elimu ya usalama na kutumia kwa usahihi alama za barabarani ili miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara za kiwango cha lami nchi iwe tija katika kuchochea usafiri na usafirishaji badala ya kuwa balaa kwa watu na mali zao.

Mkuu wa kikanda wa kituo cha umahiri wa usalama barabarani Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, Godlisten Msumanje alisema hayo mjini Kasulu katika mfululizo wa elimu kwa waendesha vyombo vya moto barabarani  yanayoendeshwa na chuo cha Taifa cha usafirishaj (NIT) ikiwa ni sehemu ya mradi wa ujenzi wa barabarani ya lami kutoka Manyovu  wilaya ya Buhigwe hadi Kabingo wilayani Kakonko mkoani Kigoma.

Alisema kuwa wakati huu miradi mikubwa ya barabara za kiwango cha lami inajengwa ajali pia zimekuwa zikiongezeka na kwamba uzembe na kutozingatia sheria za usalama barabarani imekuwa changamoto kubwa kwa waendesha vyombo vya moto hasa bodaboda na bajaji ambazo kwa sasa ndizo zinatumika kwa wingi katika maeneo mbalimbali nchini kwa shughuli za usafiri na usafirishaji.

Msumanje alisema kuwa pamoja na magari kuendelea kusababisha ajali lakini  bodaboda na bajaji zimekuwa zikishika namba kubwa kwenye ajali zinazotokea nchini na sababu kubwa ni kwa waendesha vyombo hivyo kutopitia kwenye vyuo vya udereva hivyo amewataka wamiliki wa vyombo hivyo  kuhakikisha kuwa madereva wanaoendesha vyombo hivyo wana sifa zinazotakiwa na serikali ikiwemo kupitia vyuo vya udereva na kuwa na leseni.

Akizungumza katika elimu hiyo kwa madereva Askari wa kikosi cha usalama barabarani wilayani Kasulu mkoani Kigoma, Emanuel Fusi alisema kuwa bado ipo idadi ya kutosha ya madereva wa bodaboda na bajaji ambao wanaingia barabarani kuendeshavyombo vya moto bila kupitia mafunzo ya usalama barabarani na ndiyo wanachangia ongezeko la ajali hasa wanafunzi na watoto.

Baadhi ya waendesha bodaboda na bajaji waliohudhuria mkutano huo wa kutoa elimu ya usalama barabarani wilayani Kasulu akiwemo, Emanuel Paul alisema kuwa inaweza kuwa jambo kama waendesha vyombo vya moto watabanwa kuhakikisha wanapitia kwenye vyombo ili kujua vizuri sheria na alama za barabarani ili kuzuia ajali ambapo amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya bodaboda ambao wanafanya kazi hiyo wakiwa hawana leseni.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI