Na Shemsa Mussa -Matukio daima
Kagera.
Mapendekezo hayo yalitolewa baada ya kikao Cha baraza la Madiwani Wilayani missenyi Mkoani Kagera kuchambua na kupendekeza kuwepo kwa Mabadiliko hayo.
Mabadiliko hayo yameungwa Mkono na Wajumbe wa Kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC ) inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Bi Hajjat Fatma Mwasa,ambapo wameungana na Mapendekezo ya Madiwani kutoka wilaya ya Missenyi ya kubadili jina la JIMBO LA NKENGE na Kuitwa JIMBO LA MISSENYI baada ya kujadili na kubaini sababu mbalimbali.
Zimebainishwa sababu za kubadilishwa kwa jina Hilo ikiwemo,kutokuwepo kwa mfanano wa jina la Wilaya na jina la jimbo la uchaguzi,kupelekea jina la Nkenge kutofahamika na kutotumika katika nyaraka mbalimbali za kimawasiliano baina ya Serikali,Chama,pamoja na utendaji wa Kila siku.
Pia imeelezwa kuwa jina Hilo la Nkenge limekuwa likitumika kwenye Tume huru ya Uchaguzi na uwakilishi wa Mbunge Bungeni na kupelekea jina Hilo kutumika na Mhimili mmoja wa Dola ambao ni bunge na kuacha Mihimili mingine ikiwemo Mahakama na Serikali.
Hata hivyo Madiwani hao ambao walikuwa Wajumbe katika Baraza Hilo waliweza kutoa historia ya jina la jimbo la Nkenge na kusema kuwa Nkenge ilitokana na Mto Nkenge unaopatikana Wilayani Missenyi,pia Mto huo unatenganisha Tarafa Mbili za Missenyi na Kiziba.
Kikao Cha dharura Cha kamati ya ushauri ya Mkoa (RCC) kimeitishwa ghafla leo 17 March 2025 Saa 8 Mchana katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa kagera kilichokuwa na agenda chache ikiwemo Mabadiliko ya Majina ya Majimbo ya Uchaguzi.
0 Comments