Na Hamida Ramadhan Matukio Daima app Dodoma
HOSPITALI ya Kanda ya Benjamini Mkapa imefanikiwa kupandikiza figo wagonjwa 25 kati ya 50 kwa ndani ya miaka minne kwa gharama ya milioni 875, kati ya hao wagonjwa 10 wamelipiwa matibabu hayo kupitia mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kiasi cha shilingi milioni 350.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa (BMH) professa Abel Makubi ameyasema hayo leo Machi 4,2025 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa mamlaka hiyo katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita .
Endapo wagonjwa hao wangekwenda kufanyiwa huduma hiyo nje ya Nchi Serikali ingetumia Shilingi Bilioni 1.875, hivyo kiasi cha Shilingi Bilioni 1 kimeokolewa.
Aidha, uvunaji wa figo UMEBORESHWA kwa Teknolojia ya Kisasa kwa kutumia matundu madogo (Laparoscopic Nephrectomy) ambao ulianza kutolewa Mwezi Novemba 2024 ya chini ya Serikali ya Mheshimiwa Rais Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tangia kuanza, BMH imechangia kupunguza rufaa nje kwa 99%
Kuanzishwa kwa Huduma za Upandikizaji Uloto.
Amesema mwanzoni Mwaka Jana 2023, BMH ilianzisha huduma za upandikizaji Uloto na mpaka sasa Watoto 20 waliokuwa na ugonjwa wa Sikoseli walinufaika kwa kupandikizwa Uloto na kupona ugonjwa huo ambapo kiasi cha Shilingi Bilioni 1.1 imetumika.
" Fedha hizi zimetolewa kupitia mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, na kama watoto hawa wangepatiwa huduma hii nje ya nchi ingekuwa shilingi Bilioni 2.1 , hivyo Serikali imeokoa billion 1," Amesema prof Makubi .
Amesema BMH imefanya upasuaji wa moyo kwa kufungua kifua kwa wagonjwa 60 kati ya hao watoto 38 na watu wazima 22. Kiasi cha fedha kilichotumika ni shilingi milioni 562 kati ya hizo milioni 100 zilitoka mfuko maalum wa Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan.
Aidha amesema , Watalalamu wetu wamefanya Uchunguzi wa Mishipa ya Moyo (Cardiac Catheterization) kwa wagonjwa 1173, Upandikizaji Betri wagonjwa 23, kuweka vizibua njia ya mishipa ya moyo (Stents) kwa wagonjwa 42.
"Kuanzishwa kwa Huduma za Upasuaji Upasuaji wa Ubongo na mishipa ya fahamu na unadlishaji nyonga na Magoti, " Amesema Prof Makubi
Na kuongeza "Mafanikio mengine ni pamoja na Upasuaji wa Ubongo na mishipa ya fahamu ambapo katika mika minne jumla ya wagonjwa 1061 kati yao upasuaji wa ubongo 771 na upasuaji wa uti wa mgongo 290 huku wagonjwa 440 wamebadilishiwa nyonga na magoti, " Amesema
0 Comments