Header Ads Widget

DIWANI MTITU AINGILIA KATI KASI NDOGO YA KUZALIANA KWA WANANCHI WA KIJIJI CHA KIHOMBO LUDEWA NJOMBE

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Wakazi wa Kijiji cha Kihombo kilichopo kata ya Lubonde wilayani Ludewa Mkoani Njombe wanadaiwa kupunguza kasi ya kushika mimba na kujifungua na kuongeza matumizi ya uzazi wa mpango huku sababu ikitajwa kuwa ni ugumu wa maisha na changamoto ya kufata huduma za afya za uhakika umbali mrefu jambo ambalo limetishia usalama wa kijiji hicho na kuiibua serikali ya kata kutoka na kisha kuwataka wananchi kupunguza matumizi ya uzazi wa mpango ili kunusuru kijiji hicho ambacho idadi ya wanaofariki na kuhama ni kubwa kuliko idadi ya wanaozaliwa.

Wakiweka wazi ukubwa wa changamoto ya kuzaliana inavyotishia usalama wa kijiji na hatua zilizochukuliwa,Diwani wa kata ya Lubonde Edger Mtitu na Upendo Mligo ambae ni muuguzi wakasema walilazimika kufanya mikutano na kutoa zawadi kwa wajawazito  kwasababu hali ilikuwa mbaya kwani idadi ya watu ilipungua zaidi kutokana na wengi kufariki na wengine kuhama ukilinganisha watoto wanaozaliwa.

Kituo hiki kimepata wasaa wa kuongea na akina baba na akina mama wa kijiji cha Kihombo ambapo wamesema ni kweli walisimama kupata watoto kwasababu ya ugumu wa maisha na kutokuwa na matibabu ya uhakika kijijini hapo, lakini kitendo cha diwani kuwaelimisha kimepunguza matumizi ya uzazi wa mpango.



Mara baada ya kusikia changamoto hizo,Ndipo mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga nae akaungana na diwani kuhamasisha uzazi na maboresho ya sekta ya afya kijijini hapo na barabara ambazo wananchi wanasema zinakwamisha mambo mengi kijijini hapo.

Mbunge wa Ludewa Joseph Zakarius Kamonga na Edger Mtitu wapo kata ya Lubonde kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuendelea kusikiliza kero za wananchi,kukagua miradi na kuhamasisha maendeleo.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI