Header Ads Widget

DC KIGOMA ATOA MAELEKEZO MIKOPO YA HALMASHAURI

Na Fadhili Abdallah

Mkuu wa wilaya Kigoma,Dk.Rashid Chuachua amewataka wajasiliamali waliopewa mikopo yenye thamani ya shilingi milioni 209 kutoka halmashauri ya wilaya Kigoma kurudisha mikopo hiyo kwa wakati kulingana na mikata yao na kwamba mikopo hiyo siyo sadaka wala zawadi.

Chuachua alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi mikopo inayotolewa kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani ya halmashauri ya wilaya Kigoma ambapo alisema kuwa baada ya mikopo hiyo kili kufanyiwa maboresho kwa sasa imeanza kutolewa tena kuwezesha kusaidia makundi maalum yaweze kuimarisha shughuli zao za kiuchumi kwa namna ambavyo Rais Samia Suluhu Hassan maono yake yamemuongoza katika kusaidia makundi hayo kuinua kipato chao cha kiuchumi.

Pamoja na hivyo Mkuu huyo wa wilaya alisema kuwa mikopo hiyo imelenga kuona namna wajasilimali hao wanaimarisha shughuli zao za kiuchumi na biashara na kuinua hali zao za kiuchumi na kwamba watakuwa wanafanya kosa kubwa iwapo watasindwa kurejesha mikopo hiyo kwa mujibu wa mikataba yao lakini wakidhani kwani hiyo ni  sadaka au zawadi kwao kwani kufanya hivyo kutakwamisha watu wengine Zaidi kupata mikopo.

Akitoa taarifa kuhusu utoaji wa mikopo hiyo Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashauri ya wilaya Kigoma, Judith Allute alisema kuwa mikopo yenye thamani ya shilini milioni 209.8 imetolewa kwa wajasiliamali hao ambapo jumla ya vikundi 12 vimenufaika kati yao vikiwepo vikundi saba vya wanawake na vikundi vitano vya vijana.

Afisa maendeleo huyo wa jamii alisema kuwa  mchakato wa kwa ajili ya utoaji mikopo kwa vikundi vya walemavu unaendelea na shilingi milioni 50 zimetengwa kwa vikundi hivyo.

Baadhi ya Wajasiliamali kutoka halmashauri ya wilaya Kigoma ambao wamepokea mikopo kutoka halmashauri hiyo kwa ajili ya kuimarisha shughuli zao za kiuchumi na biashara wameishukuru serikali kwa mikopo hiyo inayoonyesha dhamira ya kweli ya kuwakomboa wananchi wenye kipato cha chini.

Mmoja wa wajasiliamali hao, Zuhura Kassim kiongozi wa kikundi cha jipe moyo Mwandiga alisema kuwa wana kikundi cha cherehani na ufumaji  hivyo mkopo huo utawawezesha kunua mota za kuendeshea cherehani za umeme, mashine za kuadirizi na baadhi yam ashine ambazo zinawezesha nguo kushonwa kwa ubora kama nguo zinazotengenezwa viwandani hivyo itawasaidia  kuongeza wateja.

Naye Hungu Omari Seifu Kiongozi wa bodaboda na mabanda ya chipsi kutoka kata ya Simbo Halmashauri ya wilaya Kigoma ambao wamepata mkopo wa milioni 15 ambazo alisema kuwa watazitumia kununua pikipiki nne sambamba na kuboresha banda lao la chipsi kuwa katika mazingira ya kisasa kuifanya biashara yao kuwa na tija kubwa.

Seifu alisema kuwa ni kazi kubwa kama wangeamua kutafuta hiyo fedha wenyewe lakini baada ya kupata mkopo huo wanaamini nia njema ya serikali katika kuwainua kiuchumi itatimia na wamedhamiria kutekeleza dhamira hiyo ya serikali kwa kufaanya kazi kwa bidi kuweza kurejesha mkopo huo.



 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI