Na Mwandishi wetu Matukio Daima App.
WANANCHI wa Kitongoji cha Kisopwa kata ya Kiluvya Halmashauri ya Mji mdogo Kisarawe mkoa wa Pwani wameahidi kuwafichua waharifu watakaoharibu miundombinu ya reli ya kisasa- SGR- ili kuhakikisha inadumu kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na mtendaji wa kata ya KILUVYA ndugu Swadart Silayo baada ya kupata elimu kutoka kwa jeshi la polisi jamii kikosi cha reli walipofika kutoa elimu na kuomba ushirikiano namna ya kuhakikisha miundombinu na rasilimali za serikali ikiwemo reli -SGR- zinalindwa na kuwaibua waharifu wanaorudisha nyuma maendeleo kwa Taifa.
" Kwa niaba ya wananchi wa kata ya Kiluvya Tunashukuru kupata elimu hii mbayo ni muhimu kwa wananchi waliopo jirani na mradi wa reli ya kisasa- SGR- kuhakikisha kila mmoja wetu anatoa taarifa ya waharifu na kwa hili katika kata ya Kiluvya iwe mfano kwa wengine ili kuchukuliwa hatua za kisheria" alisema Silayo
Awali Afisa wa jeshi la polisi jamii kikosi cha reli Tanzania Kamishna msaidizi wa jeshi la polisi Acp Venance Mapala akitoa elimu ya ushirikishwaji jamii ,ulinzi na usalama wa miundombinu ya reli -SGR- kwa wakazi wa kitongoji cha Kisopwa kuhusiana na mada juu ya NANI ANAWAJIBU WA KULINDA MIUNDOMBINU YA RELI,?
Alisema kila mtanzania anawajibu wa kulinda rasilimali za taifa kwa ajili ya maendeleo yetu hivyo kitendo cha baadhi ya watu wasiowaamifu kuhujumu miundo ya reli -SGR- ni kuikosea serikali na kuisababisha harasa.
Acp MAPALA alisema kwa mujibu wa Katiba ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 27, na Sheria za serikali za mitaa sura ya 287na kwa mamlaka ya vijiji na miji sura ya 288.ambayo alielezea kwa pamoja zinamtaka mwananchi kutekeleza wajibu wa kulinda rasilimali za serikali zilizopo katika maeneo yake
"Katika sura hizo zinaelezea kuwa kila mwananchi anawajibu wa kulinda Mali zake binafsi na Mali za umma zilizopo katika maeneo yake hivyo rasilimali za umma zilizopo hapa mnawajibu wa kulinda na kutoa taarifu za wahalifu wanaotaka kukwamisha maendeleo.alisema Acp Mapala
Hata hivyo Acp Mapala aliwaomba wananchi kutoa taarifa za wahalifu na uhalifu unaotokea katika maeneo yao kwa kupiga simu namba 111 na 112 ambazo ni bure ili kuhakikisha wanashirikiana na jeshi la polisi kikosi cha Reli kwa kuchukuliwa hatua za kisheria .
Pamoja na hayo aliwakumbusha kutii mamlaka zilizopo katika maeneo yao na kulinda ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kitongoji cha Kisopwa PENDAEL MOLLEL ameshukuru jeshi la polisi kikosi cha reli kwa kutoa elimu hiyo na namba za simu ambazo hazina makato (bure ) na na kuwahidi kutoa taarifa za uharifu pale unapotokea.
Mwisho.
0 Comments