Na Fadhili Abdallah,Kigoma
wanafunzi wa shule ya Sekondari Muhange wilaya Kakonko mkoani Kigoma wameitaka serikali kusimamia kwa karibu sheria ya matunzo kwa watoto ili waweze kupata haki za matunzo na elimu waweze kutimiza ndoto zao.
Wanafunzi hao hao wametoa kauli hiyo kwa Mawakili, Wanasheria na wataalam wanaoshiriki kwenye kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia inayofanya kampeni kwa siku 10 wilayani Kakonko.
Mmoja wa wanafunzi hao,Joseph Edward wa Kidato cha nne shule ya Sekondari Muhange alisema kuwa baadhi ya wazazi wamekuwa na changamoto kubwa ya kushindwa kugharamia mahitaji ya elimu ya watoto wao ikiwemo sure,madaftari na wakati mwingine kushindwa kulipia michango hivyo mwanafunzi anasumbuka na wakati mwingine kukataa Tamara ya kuendelea na masomo.
Mwanafunzi mwingine katika shule hiyo, Adela Charles mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule hiyo alisema kuwa wanafunzi wengi wanapofaulu na kujiunga shule za sekondari wanaweka nia na dhamira ya kufanya vizuri ili kuweza kufanya vizuri waweze kupata alama ambazo zitawawezesha kujiunga na masomo ya elimu ya juu lakini wqzazi wanaposhindwa kugharamia mahitaji yao wanapatwa na msongo wa mawazo hivyo kuwa na matokeo mabaya kwenye masomo yao.Akitoa mada ya ukatili katika mkutano na wanafunzi uliofanyika shule ya Sekondari Muhange Afisa Dawati la jinsia kutoka polisi wilaya ya Kakonko, Gertrude Silvestre alisema kuwa kitendo cha wazazi kushindwa kugharamia mahitaji ya wanafunzi hao kinasababisha watoto kupatwa na msongo wa mawazo ambao ni ukatili ya kisaikolojia unaoweza kusbabisha watoto hao kufanya vibaya kwenye masomo yao.
Naye Afisa Ustawi wa jamii wa Halmashauri ya wilaya Kakonko, Meshack Kamonongo akizungumza katika mikutano mbalimbali ya wanafunzi na wananchi ikiwa ni sehemu ya kampeni ya Msaada wa sheria alisema kuwa lazime jamii ichukie ukatili wowote kwa watoto ikiwemo vitendo vya ubakaji na ulawiti, mimba kwa wanafunzi sambamba na wazazi kutelekeza familia akiwataka pia wanafunzi hao kutoa taarifa kwa vitendo vya ukatili wanavyofanyiwa au kuviona.
0 Comments