Header Ads Widget

WAANDISHI WA HABARI WAITAKA SERIKALI KUWEKA MAGARI MAALUM KWENYE MISAFARA YA VIONGOZI

Dkt.Tulia  Ackson akimjulia hali mwandishi wa Channel Ten Epimacus Apolinary aliyelazwa katika hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya baada ya kupata ajali.

Na  Matukio Daima App,

Mbeya 

UONGOZI wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Mbeya umeitaka Serikali kuweka magari  maalum kwa ajili ya waandishi pindi  wanapokua  kwenye misafara ya viongozi ili kuepukana na ajali ambazo zimekuwa zikitokea  na kuleta ulemavu wa kudumu  pamoja na vifo.


February 25,2025 Majira ya  jioni  ilitokea ajali katika  eneo la Shamwengo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya ikihusisha gari la serikali aina ya Land Cruiser mali ya ofisi ya mkuu wa mkoa Mbeya iliyokuwa imewabeba waandishi wa habari wanne na baadhi ya maofisa wa chama cha Mapinduzi.


Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari leo February 26,2025 Mwenyekiti wa klabu ya Waandishi wa  Habari mkoa wa Mbeya,Nebart Msokwa amesema ajali  hiyo iliyoua watu watatu akiwemo Mwandishi habari wa kujitegemea ,Furaha Simchimba ambao walikuwa wakitokea wilaya ya Mbarali kwenye ziara ya  Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi Taifa,Fadhili  Maganya.



"Tunaomba tunapokuwa kwenye misafara ya viongozi liandaliwe gari maalum kwa ajili ya Waandishi wa Habari ili tuweze kufanya kazi zetu za kitaaluma lakini pia tusikimbizane na misafara bila sababu huku  tukitumia magari ambayo hayana uwezo wa kukimbizana"amesema Msokwa.


Hata hivyo Mwenyekiti huyo amesema kwamba kulingana na  uzoefu waliopata wakati wa ziara ya kiongozi wa siku ya kwanza waliachwa Mbeya Vijijini wakiwa hawana gari na kulazimika kuomba kukaa kwenye gari la Mbunge wa Mbeya vijijini ambalo nalo lilikuwa limejaa na kulazimika kuomba kukaa nyuma.


"Licha ya kujibana kwenye gari hilo nyuma bado walipigwa na vumbi ambayo ni hatari kwa maisha yao lakini baada ya kulalamika siku iliyofuatwa walipatiwa gari aina ya Land Cruiser ambayo  bado hawakuwa huruma nayo kutokana na kuchanganya na baadhi ya maofisa wa chama cha Mapinduzi "amesema.


Akielezea zaidi Msokwa amesema kuwa gari hiyo iligongana uso kwa uso  na basi la Kampuni ya CRN ambayo ilikuwa ikitokea  mkoani Mbeya kuelekea wilayani Mbarali.


Aidha Msokwa  amewataja waandishi wa habari watatu waliojeruhiwa kuwa ni Epimacus Apolinary kutoka Channel Ten ambaye amejeruhiwa mguu eneo la paja pamoja na meno kutoka,Seleman  Ndelage Dreem fm ambaye alivunjika mguu na mguu na kupata majeraha mgongoni na kwenye mgongo ,Taya mwingine ni Denis George ambaye alivunjika mkono na kupata majeraha sehemu za kichwa.


"Wenzenu hawa baada ya kupata ajali walikimbizwa katika hospitali ya wilaya ya Inyala kwa ajili  matibabu na baadaye walihamishwa katika hospitaliya Kanda ya Rufaa ya Mbeya ambako wanaendelea na matibabu  na kuwa mwili Simchimba umehifadhiwa hospitali ya wilaya ya Inyala "amesema.


Aidha Msokwa ameshukuru madaktari wa hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya na Inyala kwa kuendelea kuwapatia matibabu pamoja na  ofisi ya mkuu wa mkoa wa Mbeya na ofisi ya Spika kwa ushirikiano waliounyesha.


Kwa upande wake Spika wa Bunge na Mbunge wa Jimbo la Mbeya mjini,Dkt.Tulia Ackson amepata fursa ya kufika hospitali ya Rufaa kanda ya Mbeya kuwajulia hali majeruhi ambao wanaendelea kupatiwa matibabu.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI