NA BERDINA MAJINGE MATUKIO DAIMA MEDIA ,IRINGA
MWENYEKITI wa Umoja wa wanawake wa chama cha Mapinduzi (UWT )Wilaya ya Iringa mjini Christina Makwei amewaasa wanawake wa jumuiya hiyo kutumia mitandao ya kijamii vizuri kwa ajili ya mambo ya kisiasa na sio kuwa washabiki wa kila mambo.
Makwei aliyasema hayo jana wakati wa baraza la UWT wilaya ya Iringa mjini kuwa kurekodi mazungumzo ya mtu bila ridhaa yake haifai.
"Kumrekodi mtu haifai kabisa kuwa kiongozi ukisikia umerekodiwa fatilia kimya kimya niambie nitakuletea mwanasheria ukamfungulie mashtaka,tukimuhurumia zaidi tutampeleka maadili" marufuku na haifai na haikubaliki kumrekodi mtu hasa wewe kiongozi, sijakutuma unirekodi ili umpelekee yule ningempigia nimwambie,kwenye jumuiya yangu sitaki kitu hiki kitokee kwa sababu tunaishi kwa upendo, umoja na kuelewana,naomba tusirekodiane ni mwanzo wa kutengenezeana uadui baina ya mtu na mtu"
Aidha aliwataka wajumbe hao kuacha kutegemea viti maalumu badala yake wajipange kujinadi na kupambana kwenye ngazi za uongozi na sio kusema nafasi za kugombea ni kwa ajili ya wanaume.
"Wakati ukifika nafasi haina jinsia na sisi kama wanawake tunauwezo kabisa wa kushikamana na kuhakikisha mtu akienda kwenye kata mwenye jinsia ya ke tunapambana aweze kushinda lakini tunashindwa"alisema
Makwei alisema kuwa anawaamini kwamba wanauwezo wa kusimama kwa nafasi yeyote na wakatangaza nia wakati ukifika, hivyo waende wakagombee nafasi kwa sababu hazina wenyewe.
kwa upande wake katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Mjini Hassan Makoba alisema kuwa chama cha mapinduzi kina wajumbe wanawake zaidi ya 900 hivyo wanauhakika CCM inashinda kata zote 18, na katika jimbo la Iringa Mjini.
Aidha alisema kuwa wanawake hao wanapaswa kuhamasishana kujitokeza kugombea wakati ukifika katika kata zao na jimbo na kuacha kuwa na desturi ya kukimbilia viti maalum.
"kwa sasa tunahitaji katika kata 18 nusu ya madiwani wawe wanawake,kwa sababu nia mnayo na uwezo mnayo kazi yetu chama cha mapinduzi ni kusimamia wale wanawake wenye sifa sitahiki, wakati ukifika jitokezeni hakuna kata ya mwanaume kata zote nikwa wana CCM wote wa jinsia zote"alisema
Alisema Mitano tena imeshakwisha kwa Wabunge na Madiwani mitano iliyopo ibaki kwa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,kwa madiwani na wabunge hiyo kauli isiwepo tena wagombea watashindanishwa na watapimwa kwa kazi walizofanya"alisema
MWISHO.
0 Comments