Header Ads Widget

UWANJA WA NDEGE IRINGA KUANZA ,PROF MBARAWA AMSHUKURU RAIS DKT SAMIA

  

Waziri wa uchukuzi Prof Makame Mbarawa akielekeza jambo baada ya kukagua maendeleo ya Uwanja wa Ndege Iringa 

NA MATUKIO DAIMA MEDIA 

Waziri wa uchukuzi Prof Makame Mbarawa amemshukuru Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania DKT Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha fedha kwa ajili ya upanuzi wa ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Iringa ambapo kimekamilika wa asilimia 93.

Prof Mbarawa amesema hayo leo wakati akikagua maendeleo ya ujezni huo ma kubainisha kuwa uwanja huo umekamilika kwa asilimia 93 na kutarajia febuary 22,2025 ndege ya Air Tanzania itaanza kutua rasimi katika uwanja huo.

Mbalawa alisema kuwa katika ujenzi wa kiwanja hicho cha Iringa serikali imetoa takribani bilion 68, kati ya bilion 68, bilion 63.77 ni kwa ajili ya ujenzi wa uwanja na bilion 1.77 ni kwa ajili ya kulipa fidia na bilion 2.9 ni kwa ajili ya kumlipa mkandarasi.

“Kazi ya ujenzi huo kwa asilimia 93 imekamilika ambapo uwanja huo  unaurefu wa mita  2.1 na upana wa mita 30 na uwanja huu utaruhusu ndege ya BOING, ATR 72 na nyingine za aina hiyo kuweza kutua bila matatizo”alisema.


Prof Mbarawa alieleza kuwa ujenzi huo unajumuisha njia za ndege na baadae utahusisha jengo la abiria na control tower apambo kazi yake ni kuhakikisha uwanja huo unafanya kazi kwa ufasaha, huku taa latila uwanja huo tayari zimefugwa kwa ajili ya uwanja huo utakao kuwa unafanya kazi masaa 24.

“Air Tanzania itafanya safari zake hapa mara tatu kwa wiki lakini tunaweza kuweka mara nyingi zaidi ya hapo itategemea na idadi ya abiria watakao kuwepo pia ndege za precision zitanza lufanya safari March 3,2025 na zenyewe zitafanya safari mara 3 kwa wiki, Auric Air inakuja kila siku hivyo kutakuwa na mashirika matatu ya ndege yanayofanya safari zake katika  Mkoa huo pia, flight Link itakuja ambapo itakuwa itatoa abiria Zanzibar kwenda Ruaha National Park”alisema Mbarawa

Alisema kukamilika kwa uwanja huo utafungua fursa za uchumi katika mkoa wa Iringa  wageni wengi hasa watalii watafika kwa ndege kisha watachukua magari kuelekea hifadhi ya Ruaha.

Maelekezo yangu uwanja wa ndege umekamilika hivyo wananchi mnapaswa kuulinda uwanja huu ili uweze kudumu kwa muda mrefu, pia tunaenda kuhudumia ndege nyingi na abiria wengi na abiria wamachotaka ni huduma bora wafanyakazi tumieni lugha nzuri

Watakuja wageni na watalii wengi hivyo tumieni lugha nzuri ndio itakayopeleka mbele kiwanja chetu mkitumia lugha nzuri mkoa huu utazungumzwa tanzania na nje ya Tanzania


Hivyo wale watakaopata fursa ya kuhudumia wageni tumieni lugha nzuri,ili kukitangaza kiwanja hiki n nchi kwa ujumla


Naishukuru TANROADS, TAA kwa juhudi walizozifanya katika kusimamia ujenzi wa uwanja huu na kipekee nimshukuru MH William Lukuvi kwa sababu ameanza kuupigania ujenzi wa uwanja huu tangu nimeingia katika Wizara hii ya Uchukuzi 2016 kila siku alikuwa anapambania uwanja wa ndege leo umekamilik ninaamini kuwa yupo katika furaha kubwa kuona feb 22, ndege kubwa itatua katka uwanja huu.

Akizungumzia ujenzi wa barabara ya Iringa kwenda Hifadhi ya taifa ya  Ruaha Mbarawa aliishukuru   Wizara ya ujenzi kwa kusaini mkataba wa ujenzi wa barabara inayotoka Iringa kwenda Hifadhi ya taifa ya Ruaha

Alisema hatua ya kwanza tayari imekamilika ya kusaini mkataba hatua ya pili ni mkandrasi kuleta vifaa tunaamini kama mkataba unavyosema hivi karibuni mkandarasi ataleta vifaa na kuanza ujenzi na mwisho ni kukamilisha ujenzi huo.

Kazi ya ujenzi wa barabara itachukua muda kidogo ukilinganisha na ujenzi wa viwanja vya ndege baada ya miaka mitatu barabara hiyo itakuwa imekamilika kwa asilimia 100.

Ninawaomba wale wanaopitiwa na barabara hiyo watoe ushirikiano kwa mkandarasi kumpa fursa mkandarasi aweze kufanyakazi yake vizuri ili mradi huo uweze kukamilika kwa wakati.

Akizungumzia kituo cha zimamoto katika uwanja huo alisema kuwa tayari uwanja una gari la zimamoto ambapo lazima kituo kiende sambamba na gari ili kuto huduma bora  

Alisema kuwa changamoto iliyobaki ni kujenga barabara za ukaguzi ambazo hujengwa pembeni mwa kiwanja.

Akisoma taarifa ya kiwanja hicho Meneja wa kiwanja cha ndege Iringa Ashraph Mohamed alisema kwa kiwanja hicho ni moja kati ya viwanja vya ndege 61 vinavyomilikwa, kutunzwa kuendeshwa na mamlaka ya viwanja vya ndege Tanzania (TAA)

Alisema kuwa mradi huo wa ukarabati na upanuzi wa  kiwanja cha ndege cha Iringa umehusisha ukarabati na upanuzi wa barabara ya kutua na kurukia ngede yenye urefu wa mita 2100 na upana a mita 30 kwa kiwango cha lami.

Ujenzi wa barabara ya kiungio,yenye urefu wa mita 155 na upana wa mita 23 kwa kiwango cha lami, na ujenzi wa eneo la maegesho ya ndege yenye urefu wa mita 180 na upana wa mita 126 kiwango cha lami.

Aidha mradi huo umehusisha ujenzi wa lituo cha huduma za zimamoto pamoja na ununuzi wa gari la zimamoto lenye uwezi wa kubeba lita 10,000,ufungaji wa mifumo ya taa za kuongozea ndege kwenye njia za kutua na kuruka ndege.



Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dr Linda Selekwa ambae alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa ni dhahiri upanuzi wa uwanja huo unamanufaa makubwa kwa wananchi hasa kwa wafanya biashara na ndio Mkoa ambao una hifadhi kubwa ya taifa.

Kukamilika kwa uwanja huo utaongeza wingi wa watalii katika hifadhi ya ruaha kwa kupitia uwanja huo watalii watafika kwa urahisi.

Alisema kabla ya upanuzi huo uwanja ulikuwa unapokea wageni kati ya 700 hadi 800 baada ya kukamilika uwanja huo utaweza kupokea wageni 1000 hadi 1200.

Ujio wa ndege za ATCL na Precision Air utaongeza wingi wa wageni ambapo mashirika hayo yanatarajia kuanza safari zake mwishoni mwa feb na mwanzoni mwa  mwezi march mwaka huu,ambapo ujio wa ndege hizo zitafungua uchumi wa Mkoa.

Mkoa wa Iringa kwa upande wa wilaya ya Mufindi unawafanyabiashara wengi wa mbao na wafanyabiashara hao wanajihusisha na mazao ya misitu hivyo ni fursa mpya kwa wafanyabiashara hao na tunatumai wawekezaji wataweza kuja kwa wingi na urahisi zaidi ili kuweza kuwekeza katika mazao ya misitu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI