Afisa Mwandikishaji wa Halmashauri ya wilaya ya Chalinze,Bwana Ramadhai Possi amefanya kikao na kukutana na viongozi wa vyama vya siasa kuelekea zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura utakaoanza rasmi tarehe 13-19/02/2025.
Katika kikao hicho Afisa Mwandikishaji kwa kushirikiana na Afisa Uchaguzi wa Halmashauri Bi Hidaya Maeda wametoa utaratibu wa namna jinsi zoezi hilo litakavyoendeshwa kwa mujibu wa sheria za uchaguzi wa wa Madiwani ,Wabunge na Rais pamoja na kanuni zake za uboreshaji wa daftari la wapiga kura za mwaka 2024.






0 Comments