Header Ads Widget

UTAPELI WA LBL NOMA BENKI KUU HAIJATOA LESENI WALA KURUHUSU SHUGHULI ZA LBL

Na Matukio Daima Media 

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inapenda kuutaarifu Umma kuwa haijafanya mazungumzo wala kutoa maelekezo yoyote ya kupewa leseni au kuruhusiwa kwa kampuni inayoitwa Leo Beneath London (LBL), tofauti na taarifa mbalimbali zinazosambaa mitandaoni.

Hatua za kisheria zinaendelea kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa kampuni ya LBL kwa kujihusisha na ulaghai ikiwemo kupokea amana, kutoa riba na kufanya uhaulishaji wa fedha bila leseni ya Benki Kuu ya Tanzania.

Aidha, Wananchi wanawatahadharishwa kuepuka kujihusisha na taasisi, kampuni au mtu binafsi ambaye anatoa huduma za kifedha bila kuwa na leseni ya Benki Kuu au wasimamizi wengine wa huduma za fedha.

Benki Kuu inawaonya watu na taasisi ambazo zinatumia jina la Benki Kuu kuuhadaa Umma katika vitendo vyao vya kihalifu, kuacha kufanya hivyo vinginevyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

Benki Kuu inawahimiza wananchi wanaotaka kupata huduma za kifedha kutumia taasisi zenye leseni ambazo orodha yake inapatikana kwenye tovuti ya Benki Kuu (www.bot.go.tz) au wasimamizi wengine wa sekta ya fedha nchini.

Taasisi nyingine ambazo zinatoa huduma za fedha tofauti na hizo ambazo zimesajiliwa na Benki Kuu ya Tanzania siyo halali, na hivyo Umma unashauriwa kujiepusha nazo.

Emmanuel M. Tutuba

GAVANA

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI