NA NAMNYAKI KIVUYO, ARUSHA
Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake ,makundi maalumu na watoto Dkt. Doroth Gwajima amewataka wanawake kuhudhuria katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yatafanyika mkoani Arusha Marchi 8,2025 bila kujali itikadi zao za kisiasa kwani suala hilo ni la kitaifa.
Gwajima aliyasema hayo katika mkutano
Kuelekea siku ya wanawake Duniani ambapo katika maadhimisho hayo Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.
Alisema suala hilo sio la kichama bali ni suala la kitaifa hivyo wanawake wasijifungie ndani kwaajiljili ya itikadi za kisiasa, wajitokeze kusherekea mapinduzi makubwa ya wanawake katika uongozi lakini pia kupata elimu juu ya masula mbalimbali ya kiafya, kiuchumi na kijamii.
Aidha alifafanua kuwa wameamua kufanyia maadhimisho hayo Arusha ili kutoa msukumo kubwa wa elimu kwa umma ili kubadilisha sura ya takwimu za masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukatili.
"Nikisema hivi sio kwamba Arusha kuna masuala ya unyanyasaji kila mtu ananyanyasika hapana, ila kuna makundi ambazo unakuta kwasababu zingine ikiwemo imani, mila na desturi wanakuwa wamebaki nyuma wanafanya vitu fulani kinyume na ulimwengu wa sasa unavyotaka unavyotaka na kujiweka kwenye hatari bila wao kujua," Alisema
"Tunataka tuwawekee mkakati wa kuweza kuwafikia katika elimu ili kuwakomboa fikra zao ili wawende sambamba na mahitaji ya ustawi wa maendeleo kwa zama za sasa kama wezao mfano mkoa wa Mara walikuwa wanaongoza kwenye masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na ukeketaji wa watoto lakini tumewekeza katika elimu na sasa imepungua na kutuachia Arusha na Manyara," Alieleza Gwajima.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Arusha Paul Makonda alisema kuwa wameamua kufanya sherehe hizo ndani ya siku 7 kwanzia march1,2025 ili kuongeza maana na tija kwa wananchi ambapo kutakuwa na huduma mbalimbali zitakazo tolewa ikiwemo Afya, Elimu, maonyesho pamoja na michezo na burudani.
"Kwenye suala la huduma tumeona ni vema tutumie fursa hii kwa wananchi wa mkoa wa Arusha kupata huduma ambazo kwao zinakuwa kama kero au changamoto na hatimaye kufika hatua ya kuilaumu serikali au kuona hakuna maana ya kufurahia wakati mioyo yao ina huzuni ,"Alisema Makonda.
Alifanua kuwa mambo hayo yamejikita sana kwenye masualanya ardhi ndio sababu kubwa ya kuomba wizara ya katiba na sheria kupitia programu ya Samia Legal Aid kuja katika mkoa wetu wa Arusha na kuanza kutoa huduma kwanzia tarehe 1.
Mwenyekiti wa hamasa mkoa wa Arusha Bi Hindu Mbwego alisema kuwa walikadiria kupata watu 400,000 lakini mpka sasa wameweza kuwafikia watu 700,000 zikiwemo jamii za pembezoni (wamasai, waberbeig) wageni 100 kutoka nchi za nje pamoja na wawakilishi wa jumuiya mbalimbali zikiwemo za dini.
"Pamoja na hayo pia tutakuwa na akina baba zaidi ya 1000 wanaotuunga mkono ambao wataitwa baba wa zamu lengo likiwa ni kuonyesha tutakavyoshirikiana pamoja katika kulea watoto ili kuwa na familia zilizo kamilika,"Alisema.
Mwakilishi wa kamati ya michezo Amina Mosha alisema kuwa wameshaanza mashindano ya kupata timu bora itayowakilisha mkoa katika mashinda ya kitaifa lakini pia kutakuwa na mbio zitakazoshirikisha wanawake zaidibya 500 pamoja na kuwepo kwa michozo ya asili kama vile mdako na rede.
0 Comments