Header Ads Widget

SINTOFAHAMU UENYEKITI WA BARAZA LA UONGOZI CHUO KIKUU IRINGA

                  Dkt Lilian Badi 

KATI ya maswali ambayo wanajiuliza baadhi ya wanazuoni chuo Kikuu Cha Iringa ni juu ya nafasi ya Mwenyekiti wa Baraza la uongozi chuo Kikuu Cha Iringa.


Jina la Dkt Lilian Badi kwa safu ya uongozi wa chuo Kikuu Cha Iringa naweza kusema ni jina kubwa ndani ya chuo hiki Iringa .


Pamoja na jina hili kuwa maarufu kutokana na nafasi yake ndani ya chuo hicho ila yapo maswali Binafsi nimekuwa nikijiuliza nakosa majibu ya Moja kwa Moja .


Kwani hakuna ubishi kama safari ya Lilian ilianza katika chuo hiki kwa kuwa mmoja kwa wahitimu wake wa liofanya vizuri na hata kikishawishi chuo kumpa nafasi ya kuwa keshia ndani ya chuo .

Dkt Lilian alipata nafasi ya kuwa keshia baada ya kuhitimu Diploma ya uhasibu  ya chuo hicho Cha Iringa ambapo ajira yake alianza mwaka 1993.


Miaka Mitatu baadae alihitimu Digirii ya uzamivu wa biashara na baada ya hapo cheo kikapanda na kuwa Msaidizi wa mtunza hazina .

Lilian Badi Miaka mitano baadae cheo kikapanda baada ya kuwa na shahada ya udhamili .


Mwaka 2011 aliomba kwenda kusoma shahada ya juu ya uzamivu ambayo hakwenda kabisa kusoma pamoja na kulipwa kwenda kusoma kwa Miaka 6.


Hivyo Miaka yote 6 alikuwa akipokea mshahara na akiulizwa hakuwa mkweli kwanini hajaenda kusoma na mshahara anapokea.


Mwaka 2016 chuo kiliamua kumfukuza kazi baadae kwa ajili ya sababi Binafsi ambayo haijulikani uongozi wa chuo ulimteua kuwa mjumbe wa Baraza la uongozi hapa ni kati ya mwaka 2017-2021 akiwa nafasi ya makamu mwenyekiti wa mkuu wa chuo .


Mwaka 2022 aliteuliwa kuwa mwenyekiti wa Baraza la uongozi wa chuo Kikuu Cha Iringa.


Sina shaka na kupanda kwake kwa uongozi ila najiuliza maswali yasiyo na majibu hapa.


Inakuwaje mtu aliyeshindwa Masomo ya uzamivu awe mwenyekiti wa wasomi kama Madaktari na Maprofesa ambao wamesoma zaidi yake na si Wababaushaji wa elimu?


Kama haitoshi iweje mtu aliyefukuzwa na Taasisi hiyo hiyo kwa Kukosea misingi na taratibu ikiwemo tuhuma za kukiibia chuo kwa kulipwa mshahara bila kwenda masomoni kwa Miaka 6 Leo kuwa kiongozi wa juu hivi ana sifa zipo za kusimamia chuo kama mwenyekiti wa Baraza la uongozi?


Maswali haya Pekee yanafikirisha sana kwa chuo chenye malengo Makubwa ya kitaaluma kuwa na mtu kama huyu ndio maana changamoto za chuo haziishi kwani mwenyekiti wake ni changamoto moto.


Ninaomba Maswali haya baba Askofu Dkt Blaston Gavile asaidie kunipa majibu kama hivi ndivyo chuo kinavyotaka ama lah!


Pia niulize bodi ya Udhamini mlimteuaje mtu aliyefeli Kuongoza watu waliofaulu?


Hivi ni kweli mlikosa mtu kabisa mwenye sifa ndani ya chuo hiki Bora chenye sifa Kuongoza bodi ya watu wenye sifa.


Nimemtaguta Lilian Badi ili anisaidie majibu ya maswali yangu nimemkosa ila nimefanya jitihada za kumtafuta  baba Askofu Dkt Blaston Gavile pia sijampata jitihada zinaendelea .


Simu ya Askofu mstaafu wa kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT)Prof   Owdenburg Mdegella haijapatikana na watu wa Jirani wanadai yupo nje ya nje hivyo nitamtafuta Pindi atakaporejea nchini ili kupata majibu haya .

Japo vyanzo vya kuaminika vimenidokezea barua nyeti za kufukuzwa kwake tutaziachia hapa 

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI