MKUU wa Mkoa wa Pwani Abubakar Kunenge amewataka wananchi kutumia kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia kutatua changamoto za kisheria
Kunenge ameyasema hayo Mjini Kibaha wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya siku tisa ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Mkoani Pwani.
Amesema kuwa kampeni hiyo ni nzuri na itawasaidia wananchi wanyonge ambao hawana uwezo wa kulipia gharama za kisheria.
Naye Naibu Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalum Mwanaid Khamis alisema kuwa kumekuwa na changamoto ya ukatili wa kijinsia, matunzo ya watoto, ardhi na ubakaji.
Mwakilishi wa bodi ya ushauri wa msaada wa kisheria Nuru Awadh alisema kuwa siku tisa ni chache kwani changamoto ya masuala ya kisheria ni kubwa sana hivyo ili kuwafikia wananchi wengi hivyo huduma ziendelee kutolewa.
Mkurugenzi wa mashirika yanayotoa msaada wa kisheria (TANLAP) Christina Ruhinda alisema kuwa kila kata ina wasaidizi wa kisheria nchi nzima ambao wanasaidia kutoa elimu na msaada wa kisheria.
0 Comments