Na Leonard Johnson ,Matukio Daima Media Iringa
ASKOFU wa kanisa la kiinjili la kilutheli Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mufindi Dkt.Antony kipangula Amewataka vijana kuacha kutegemea kutafuta pesa kupitia mitandao ya simu kama Kubeti na LBL badala yake wajikite kufanya kazi ambazo zinaweza kuwaingizia kipato halali.
Kuwa Kasi ya Vijana na baadhi ya watanzania kushinda kwenye mitandao kutafuta pesa ni kubwa Kuliko Ile ya kufanya kazi za uzalishaji mali kama Kilimo na nyingine .
Askofu Dkt Kipangula alisema ni vema mitandaoni kuingia baada ya kutoka Shamba kulima na isiwe kazi ya kuingiza kipato .
Askofu Dkt Kipangula alisema hayo Jana wakati wa Ibada ya uzinduzi wa Jimbo la Nyanyembe wilaya ya Mufindi Mufindi Mkoani Iringa na kumuingiza kazini mkuu wa Jimbo hilo Mchungaji David Nyambulapi .
Aliwataka wazazi Kuwahimiza watoto kufanya shughuli ambazo serikali ina weza kushirikiana nao ,shughuli hizo kama vile elimu na taasisi za malezi na kuepukana na kazi zisizo kuwa na uhalali hasa michezo hiyo ya kubashiri mitandaoni .
Pia kutumia nguvu kazi za kujiingizia kipato na kuepukana na na uvivu ,jambo ambalo litawafanya kuepukana na kufanya kazi za utapeli hasa mitandaoni ,jambo ambalo linaweza kuleta mmomonyoko wa maadili na kuzuia maendeleo ya nguvu kazi .
Hata hivyo aliwataka wataka wabunge pamoja na viongozi wa dini kuungana pamoja Katika maswala mbali mbali ya kijamii,kiuchumi na kisiasa katika kudumisha amani na maendeleo ya Taifa,kwani wao wanaweza kuwa chachu kwa jamii .
Dkt.Kipangula alitoa wito kwa jamii kujikita katika ubunifu na kujibidiisha katika kutumia fursa zilizopo katika mazingira wanayoishi mfano kutumia fursa ya kilimo kama ajira na sio adhabu .
"Hii nikutokana kwamba jamii nyingi za kitanzania zina amini kwamba kilimo ni adhabu ya walio shindwa kusoma na sio ajira jambo ambalo huleta umasikini"
Alisema ni lazima watu kutumia fursa zilizopo na pia kuacha uvivu na lazima kutumie nguvu na tufanye kazi kwa jasho .
Kuwa kuna watu hawataki kutumia nguvu wanataka vitu rahisi sana unakuta mtu anakaa na simu yake anaingia mtandaoni anatapeli hata mamilioni kuwa huo ni uhalifu kabisa lazima jamii ibadilike ijitumii.
0 Comments