Header Ads Widget

SERIKALI YAGAWA PIKIPIKI KWA AJILI YA KUIMARISHA HUDUMA ZA CHANJO MKOANI SONGWE.

 

Na Moses Ng'wat, Songwe.

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Kitengo cha Chanjo, imegawa pikipiki tisa aina ya Yamaha kwa halmashauri za Mkoa wa Songwe ili kuboresha usambazaji wa chanjo na vifaa vyake katika vituo vya afya.


Zoezi hilo limefanyika Februari 26, 2025 katika hafla fupi iliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Songwe na  kusimamiwa na Katibu wa Afya wa mkoa huo, Uswege Mwaipungu, kwa niaba ya Mganga Mkuu wa Mkoa.

Akizungumza katika hafla hiyo akiwa ameambatana na pamoja na wajumbe wa timu ya Usimamizi wa Huduma za Afya ya Mkoa (RHMT), Mwaipungu alisema kuwa, 


Hatua ya serikali kugawa pikipiki inalenga kuongeza ufanisi wa utoaji wa chanjo na kuimarisha ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.


"Serikali inaendelea kuwekeza katika sekta ya afya ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na kwa wakati.



"Tunatarajia pikipiki hizi zitasaidia kuongeza kasi ya usambazaji wa chanjo, hasa maeneo ya vijijini," alisema Mwaipungu.


Katika mgao huo, kila halmashauri ya wilaya imepokea pikipiki mbili, huku Halmashauri ya Mji wa Tunduma ikipokea pikipiki moja. 


Mwisho.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI