Header Ads Widget

ONYO KALI KWA WANAOHARIBU MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU DAKAWA,MAZIMBU NA MAENEO MENGINE KWA KUONDOA ALAMA

 






Na Lilian Kasenene, Morogoro
Matukio DaimaApp 

WAZIRI wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Prof Palamagamba Kabudi, amelitaka jeshi la polisi na mamlaka nyingine za kisheria kuchukua hatua kali dhidi ya wahalifu wanaoharibu na kuiba alama za makaburi ya wapigania uhuru wa Afrika Kusini eneo la Dakawa, na maeneo mengine nchini kwani ni kuiondolea heshima nchini.

Katika ziara yake mkoani Morogoro eneo la urithi wa kihistoria,Waziri Prof Kabudi, alisema kuwa vitendo hivyo vinatia aibu kwa Taifa na ni sawa na kufuta historia muhimu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa Afrika.

Waziri Prof Kabudi aliagiza kukamatwa na kufikishwa mahakamani bila huruma watuhumiwa wote wanaohusika n kufanya hujuma hizo kwani kwa Sheria ya maeneo yanayolindwa sura ya 74 ya nchi adhabu yake ni miaka 30.

"Nadhani wakikamatwa wawili au watatu kwa kuvunja mawe watu watajifunza, tuyaheshimu makaburi
ya Hawa ndugu zetu,"alisema.

Mbali na kuchukua hatua za kisheria, Waziri Kabudi alieleza kuwa Serikali ina mpango wa kuyasajili maeneo ya kihistoria 260 , ikiwemo Dakawa, Mazimbu, Mgagao, Nahingwea na Bagamoyo, ili yawe sehemu ya Urithi wa Dunia. Lengo ni kuongeza thamani ya urithi wa kihistoria.






Alisema serikali imeanza jitihada ya baadhi ya maeneo hayo kiingizwa kwenye kumbukumbu na kuwa sehemu ya urithi wa Dunia chini ya Shirika la Umoja wa mataifa la Sayansi, Elimu na Utamaduni(UNESCO), ambapo alitolea mfano kwa nchi za Afrika Magharibi ambapo maeneo yote yaliyokuwa ya watumwa yaliingizwa kwenye urithi huo.

Pia alisema Wilaya ya Kilosa itakuwa kitovu cha utalii wa historia hivyo maeneo kama Dakawa ni vyema ikalindwa.

Aidha alieleza kuwa Tanzania ina malengo mawili ya kuhakikisha yanakuwa kwenye urithi wa Dunia kihistoria ambayo ni kuwa kwenye orodha ya urithi wa kimataifa na urithi wa kimataifa usioshikika na kwamba 

Pia, Waziri Kabudi aliagiza kupigwa Picha makaburi yote ili kuwepo kwa  kumbukumbu na kutengeneza ramani makaburi yote na kuyatunza.

Baadhi ya wananchi mkoani Morogoro walizungumzia namna alama za makaburi yanavyo haribuwa, walisema hilo limekuwa tatizo kubwa na wahalifu wamekuwa si wahiga.

Petry Robert mkazi wa Mazimbu alisema suala la ulinzi na usalama kwa makaburi kwa ujumla ni jambo ambalo linatakiwa kuwekewa mkakati mahususi kama kujengwa kwa uzio kwenye maeneo yote ya makaburi yakiwemo ya wapigania uhuru.

"Ni imani yangu kuwa na uzio tutaweza kuthibiti wizi wa misalaba iwe kwa maeneo yotee,"alisema

Mwisho..




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI