Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe.Antony Mtaka akikabidhi Hundi kwa makundi ya wanawake,Vijana na wenye ulemavu
Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Zaidi ya shilingi bilioni 1.1 zimetolewa kwa vikundi 92 vya wanawake,Vijana na walemavu katika Halmashauri ya wilaya ya Njombe ili zikawasaidie kuendesha miradi mbalimbali Fedha ambazo hutolewa kupitia makusanyo ya mapato ya ndani.
Fedha hizo ni zile za Asilimia kumi za maelekezo ya serikali ambazo awali zilisitishwa kutokana na changamoto mbalimbali zilizoibuka ikiwemo ukiukwaji wa utoa na baadhi ya viongozi wakiwemo Madiwani kunuifaka nazo ili Hali sio walengwa.
Taarifa ya utoaji mikopo hiyo iliyosomwa na Ofisa Maendeleo Halmashauri ya wilaya ya Njombe Sarah Chambachamba imesema safari hii Wametoa kwa vikundi vilivyokidhi vigezo.
Mbunge wa Jimbo la Lupembe Edwin Swalle na Justin Nusulupila Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Njombe wamewataka waliopata Fedha hizo kwenda kuzitumia kwa kadri ya malengo na sio kuzifuja.
Akikabidhi Hundi hiyo Mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka Amesema anataka kuona matokeo chanya katika Fedha hizo kwa vikundi vyote huku Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Njombe Deo Sanga akiwaonya na tabia ya kutumia fedha hizo kwenye pombe na starehe nyingine.
Baadhi ya wananchi wilayani Njombe waliopata mkopo huo wameahidi kwenda kuendesha biashara na ujasiriamali waliopanga kuutekeleza kwa umakini mkubwa.
0 Comments