Header Ads Widget

MWENYEKITI MTAA WA MUUNGANO GOBA AANZA KWA KISHINDO

 

Na Mwandishi Wetu


MWENYEKITI wa Mtaa wa Muungano kata ya Goba Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam, Isack Maduhu ameanza kazi kwa kusambaza mabomba ya maji.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa mkutano wa wananchi na kuwashukuru kwa kumchagua, Maduhu alisema suala la maji limepata ufumbuzi kwa kuwa tayari mabomba yamesambazwa na wananchi wanahimizwa kujaza fomu za maombi ya huduma hiyo.

"Wananchi wameanza kuchukua fomu za maombi ya kuunganishiwa maji na mabomba yamekabidhiwa katika shina namba nne na shina namba tano," alisema Maduhu.



Mwenyekiti huyo anayepeperusha bendera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) alisisitiza kwamba mchakato wa ujenzi wa zahanati ya mtaa unaendelea huku akiamini kwamba itakapokamilika itarahisisha upatikanaji wa huduma za afya karibu na wananchi.

"Mchakato wa zahanati ni wa miaka mitano, ulianza mwaka 2024 tnatarajia hadi 2029 utakuwa umekamilika kwa kuwa hii pia ni sera ya CCM kuhakikisha kila mtanzania anapata huduma bora za afya karibu nae... tukiwa na jamii yenye afya bora ni rahisi kupata maendeleo," alisisitiza Maduhu.


Kuhusu elimu mwenyekiti huyo alisema atatembelea shule za awali, msingi na sekondari zilizopo kwenye mtaa wake bila taarifa ili kuona hali halisi ya upatikanaji wa huduma hiyo muhimu na ubora wa majengo.


Katika mkutano huo wa wananchi Mwakilishi wa TARURA, Injinia Cavine Lugendo alisema ofisi yake imeomba fedha kwa ajili ya kutengeneza maeneo yaliyoharibiwa na mvua hasa madaraja madogo ualiyopo kwenye mtaa huo wa Muungano Goba.


Injinia Lugendo alisema ameyatambua maeneo korofi na kuahidi kuanza nayo pindi atakapopata fedha kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Ubungo.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI