Na Matukio Daima media
Mkuu wa wilaya ya Kisarawe Petro Magoti amepokea msaada wa mabati 400 kutoka banki ya NMB yenye thamani ya shilingi milioni 16 kwaajili ya shule 14 za msingi na sekondari wilayani humo na kuahidi msaada huo utachochea ufaulu wa wanafunzi wilayani humo.
Akipokea msaada huo ofisini kwa Mkuu wa Wilaya Kisarawe mkoani Pwani kutoka kwa Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Seka Urio ambapo Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ameshukuru banki hiyo ya NMB na kuahidi shule zitakazopata mgao wa mabati hayo atasimamia wafanye vizuri masomo yao.
Aidha amesema atawachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kuwapangisha kwenye nyumba zao wanafunzi anatarajia kuanza operasheni maalumu ya kurudisha hosteli wanafunzi waliopanga nyumba za kuishi mitaani ili kuhakikisha usalama wao.
Magoti amesema mheshimiwa Rais amejenga hosteli zakutosha hakuna sababu ya wanafunzi kupanga vyumba mitaani na kuingia gharama kubwa huku serikali imeshagharamia hosteli kwaajili yao.
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es salaam Seka Urio amezitaja shule za sekondari zitakazopata mabati hayo kuwa ni shule za Sekondari Suleiman Jafo, Jokate Mwegelo na Kisangireza na kushukuru kwa kushirikiana na Banki hiyo katika mambo mbalimbali hususani masuala ya maendeleo ya jamii.Seka amesema Banki ya NMB changamoto za sekta ya elimu Tanzania ni jambo la kipaumbele, hii ni kutokana na ukweli kwamba Elimu ndio ufunguo wa maisha na maendeleo kwa taifa letu.
“Tunatambua juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan za kusimamia upatikanaji huduma bora za Elimu kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mjini na vijijini; hatuna budi kuipongeza Serikali kwa hilo alisema Seka.
“Vifaa hivi tunavyo kabidhi leo ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii na sisi kama benki inayoongoza Tanzania, tunao wajibu wakuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika kutokana na faida tunayoipata”.
“Benki NMB tumekuwa mstari wa mbele kuchangia huduma za kijamii kwa lengo la kurejesha sehemu ya faida yetu kwa jamii. Ni kwa zaidi ya miaka nane mfululizo tumekuwa tukitenga asilimia 1 ya faida yetu kama sehemu ya uwajibikaji kwa jamii inayotunzunguka alisema Seka.
Kwa taarifa tu, Benki NMB ndiyo benki inayoongoza nchini huku tukiwa na matawi 231 Tunamashine za ATM zaidi ya 700 nchi nzima, NMB Wakala ni zaidi ya 40,000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 7 idadi ambayo ni hazina kubwa ukilinganisha na benki nyingine hapa nchini.
0 Comments