Header Ads Widget

WANANCHI LINDI WAKUMBUSHWA UMUHIMU WA KUANDIKA WOSIA

 


Wananchi Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi wametakiwa kuacha dhana potofu ya kuhusisha wosia na uchuro badala yake wametakiwa kufanya hivyo ili kuepusha migogoro ya Mali mara baada ya kufaliki


Hayo yameelezwa na Afisa aridhi Mteule wa Manispaa ya Lindi na Mjumbe wa kamati ya kampeni ya Msaada wa kisheria inayoendelea Katika Manispaa hiyo  February 23,2025 alipokuwa anazungumza na wananchi waKijiji cha Moka , Likwaya na Matimba 

 Munisi alieleza kwamba  Watu wengi wamekuwa na dhana potofu kwamba wosia ni jambo la uchuro au linalohusiana na kifo, jambo ambalo si kweli.

amesema wosia ni hatua muhimu kwa kuhakikisha mali na mali ya familia zinagawiwa kwa haki na kwa usawa baada ya kifo  cha mmiliki. 

Aidha, aliwasisitizia wananchi kuhusu faida za kuwa na wosia, ikiwa ni pamoja na kuepuka migogoro ya kifamilia, kulinda haki za watoto, na kuweka mipango bora kwa familia wakati mtu akiwa hai.

Pia, alieleza mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kuandika au kuacha wosia, ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri wa kisheria, kuhakikisha kuwa wosia umeandikwa kwa njia ya kisheria, na kuhakikisha kwamba una saini ya mashahidi waliothibitishwa ili kudhihirisha kuwa ni halali.

Aliwahimiza wananchi kuwa na ujasiri wa kuandika wosia, kwani ni hatua muhimu ya kuwa na amani ya kisheria na familia bora baada ya kifo.

Afisa usawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo bwana Kasimu Mkwili amesema  kutokana na wosia  aliouancha Marehemu akiwa hai unaweza kumtambua Hata Mtoto akizaliwa nje ya ndoa Hata kama hatambuliki na familia .

" Mfano Katika Sheria za duni ya kiislamu Mtoto wa nje ya ndoa hatambuliki Katika Mali za Marehemu endapo ndugu hawakuweza kumtambua Mtoto huyo kabla ya kifo chake lakini kupitia wosia Mtoto Yule anaweza kumrithi Mzazi wake Hata kama hakutambulika kabla " alisema Mkwili 

Bwana Juma Mbarouk ni Mkazi wa Moka amesema kupitia Elimu hiyo na Elimu mbalimbali zilizotolewa na timu hiyo ya wataalamu wa msaada wa kisheria wananchi wamefurahishwa kwa kufahamishwa maswala hayo na kwamba wamejifunza vya kutosha .








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI