Header Ads Widget

RAIS DKT SAMIA AZINDUA JENGO LA HALMASHAURI YA BUMBULI TANGA ATAKA WANANCHI KULITUMIA KUPATA HUDUMA BORA

 

Na Matukio Daima Media 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Jumatatu Februari 24, 2025 amezindua Jengo la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli Mkoani Tanga akihimiza utoaji wa huduma bora kwa wananchi watakaokuwa wanafika kwenye Jengo hilo kupata huduma mbalimbali za serikali.


Katika Hotuba yake fupi kabla ya kuelekea Wilayani Lushoto Mkoani Tanga alipopangiwa kufanya Mkutano wa Hadhara Leo Jioni, Rais Samia pia amewataka wananchi wa Wilaya ya Bumbuli kulitumia Jengo hilo kikamilifu kuweza kupata huduma zitakazokuwa zinatolewa Kwenye Jengo hilo la Halmashauri hiyo, akiwapongeza pia wakandarasi na wasimamizi mbalimbali waliosimamia Jengo hilo.


Katika ziara hiyo Rais Samia Suluhu Hassan amesisitiza kuwa Ujio wa ziara yake Mkoani Tanga ni kuja kuangazia matumizi ya gharama za fedha takribani Trilioni 3.1 zilizotolewa na serikali kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani Tanga, ikiwa zimefanya kazi iliyokusudiwa na serikali.

Jengo hilo la Halmashauri ya Wilaya ya Bumbuli lina vyumba 72 vya watumishi na wakuu wa idara zote za Halmashauri ya Bumbuli pamoja na Kumbi za mikutano sambamba na miundombinu mbalimbali ya huduma kwa wenye mahitaji maalum na Gharama za ujenzi wa jengo hilo ni shilingi Bilioni 6 zikitajwa kusaidia katika kurahisisha na kuboresha huduma kwa wananchi.


TAZAMA FULL VIDEO BOFYA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI