Na Fatma Ally Matukio DaimaApp
Mapambano 14 ya ngumu kushuhudiwa leo usiku katika Viwanja vya Magomeni Sokoni ambapo Men Card wa Mchezo huo Amiri Matumla kutoka Tanzania na Paul Amavila kutoka Namibia.
Knock Out ya Mama msimu wa tatu imekuja kivyengine ambapo wameanza kwa kugawa majiko ya gesi kwa wamama Ntilie wa magomeni sokoni ambapo zoezi hilo litakua endelevu.
Pambano hilo litafanyika leo Februari 28, 2025 jijini Dar es Salaam likihusisha mabondia kutoka ndani na nje ya nchi ambapo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam anatarajia kuwa mgeni rasmi.
Kuelekea mapambano hayo jana kulikuwa na zoezi la kupima uzito na face-off kwa mabondia wanaotarajiwa kushuka ulingoni katika mapambano ya raundi sita na nane, yakiwemo yale ya main event.
Akizungumza wakati wa zoezi la face off Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion, Ally Zayumba, amesema kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia kama gesi na umeme badala ya kuni na mkaa.
Baadhi ya wanawake waliopokea mitungi hiyo walielezea furaha yao kwa hatua hiyo na kupongeza Mafia Boxing Promotion kwa kuona umuhimu wa kusaidia jamii na kuunga mkono sera ya Serikali ya Awamu ya Sita kuhusu nishati safi ya kupikia.
Katika zoezi la kupima uzito, Rashid Matumla, bondia mstaafu na baba wa Amiri Matumla, ambaye anapigana kwenye main card, alisema kuwa mwanawe amejiandaa vizuri na ana nidhamu ya hali ya juu ndani na nje ya ulingo.
Kwa upande wake, Amiri Matumla aliahidi kutoa ushindi mnono dhidi ya mpinzani wake, Paulo Amavila kutoka Namibia, huku Amavila akijigamba kuwa Matumla bado ni mdogo kwake na hana nafasi ya kushinda.
Naye Promota mkongwe, J. Msangi, aliwapongeza Mafia Boxing Promotion kwa jitihada zao katika kuendeleza mchezo wa ngumi, akisema kuwa wao walifungua njia na sasa Mafia Boxing wanaendeleza kwa kiwango cha juu, huku akitabiri Tanzania kupaa zaidi kimataifa katika masumbwi.
Msimu wa tatu wa Knock out ya mama umekua wa kipekee zaidi ambapo mabondia wenye uwezo watapanda ulingoni kutoa burudani ya kutosha.
0 Comments