Header Ads Widget

JIMBO LA SAME MASHARIKI LINAVYOCHANJA MBUGA KATIKA SEKTA YA AFYA..



NA WILLIUM PAUL, SAME.



SEKTA ya Afya ni sekta muhimu katika Taifa lolote Dunia lenye lengo la kukuza maendeleo ya wananchi wake na Taifa kwa ujumla kwani ili Uchumi ukuwe ni lazima wananchi wawe na Afya njema.


Nchini Tanzania Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani imekuwa ikitekeleza kwa vitendo sekta hii kwa kutoa fedha nyingi kuboresha huduma ya Afya na kuifanya kuwa karibu zaidi na Wananchi.



Wakati Mama huyu anaingia madarakani kuchungua uongozi Jimbo la Same mashariki lililopo wilayani Same mkoani Kilimanjaro lilikuwa na jumla ya kituo kimoja cha afya ambacho ni cha serikali Ndungu.


Mbali ya uwepo wa vituo hivyo lakini vilikuwa havijitoshelezi kutokana na kukosekana kwa baadhi ya huduma muhimu hali ambayo ilikuwa ikiwalazimu Wananchi kwenda katika mkoa wa Tanga kupata huduma huku wangine wakitembea kilomita zaidi ya 100 kufuata huduma katika hospitali ya wilaya ya Same.



Kama wasemavyo wahenga “Uchungu wa mwana aujuae mzazi hasa Mama” ndipo Mbunge wa Jimbo hilo mwanamama shupavu Anna Kilango Malecela alipoamua kuibeba agenda ya afya na kuifanya kama agenda ya kipaombele na kuifikisha Bungeni kuipigia kelele.


Kelele za mama huyu zilimfikia Mwanamama mwenzake na kiongozi mchapakazi mwenye maoni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo aliamua kujibu agendo hiyo kwa vitendo kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa vituo vipya vya Afya vya Miamba, Mtii na Vunta.



Mbali na ujenzi wa vituo hivyo lakini Dkt. Samia aliamua kutoa fedha kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika vituo vya Afya vya Ngundu na Mtii pamoja na kujenga Majengo mapya na kuhakikisha huduma zote muhimu zinatolewa katika vituo hivyo.


Hatua hii imekuwa neema kubwa kwa Wananchi ambao walikuwa wakisafiri kutoka umbali mrefu zaidi ya kilomita 100 kufuata huduma za afya mkoa wa Tanga huku wengine wakienda Same.



Rashid Juma ni mkazi wa kata ya Bwambo anadai kuwa, hapo awali wananchi wengi walikuwa wakifariki dunia kutokana na huduma za afya kuwa mbali na maeneo yao hali ambayo ilikuwa ikiwalazimu kutumia fedha nyingi kufuata huduma za afya.


Anasema kuwa, tatizo hilo lilikuwa kikwanzo kikubwa hasa kwa Wakinamama wajawazito ambapo wakati mwingine walikuwa wakilazimika kujifungulia nyumbani au njia.



“Sasa hivi tunaweza kusema tupo katika dunia nyingine kabisa kwani serikali imetuboreshea huduma za afya kwa kiasi kikubwa kwani sasa hiki kila Tarafa inayo kituo cha Afya kikubwa kinachotoa huduma zote muhimu hatuagaiki tena kutumia gharama kubwa kufuata huduma za afya” anasema Juma.


Mbali na serikali kuwekeza katika vituo vya afya lakini pia imewekeza katika zahanati na kuhakikisha vifaa tiba na dawa muhimu hazikosekani katika ngazi hiyo huku wananchi wakihudumiwa kwa gharama nafuu ambayo kila mmoja anaweza kuimudu.



Hili tunaweza kusema kuwa, Mbunge wa Jimbo la Same Mashariki, Anna Kilango Malecela na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wanaupiga mwingi katika sekta ya Afya katika jimbo la Same mashariki.


Mwisho…

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI