Header Ads Widget

MAKONDA AWATAKA WAKAZI WA MKOA WA ARUSHA KULINDA AMANI ILIYOPO.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amewataka wananchi wa Mkoa huo kuendelea kulinda na kuitunza amani iliyopo ili nchi kuweza kupata kipato kupitia utalii wa mikutano na mtu mmoja mmoja kunufaika.

Makonda ametoa kauli hiyo leo katika kikao kazi cha Maandalizi ya Siku ya wanawake Duniani ambayo kitaifa yatafanyika jijini Arusha,kilicholenga kuweka mikakati ya kuhakikisha maadhimisho hayo yanafanyika kwa ufanisi Mkubwa.

Akizungumza katika kikao kazi hicho amekemea watu baadhi ambao wananufaika na fedha zinazotokana na ushoga ambapo ameziomba taasisi za dini,kijamii na asasi za kiraia pamoja na mtu mmoja mmoja kuendelea kukemea vitendo hivyo.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, jinsia,wananwake na makundi maalum,anayeshughulikia wanawake na jinsia Felista Mdemu katika kikao kazi hicho amesema Wizara kama waandaaji wakuu wa maadhimisho hayo kuanzia machi mosi hadi 7 itakuwa ni wiki ya mwanamke itakayoambatana na utoaji wa elimu kwenye nyaja mbalimbali.

Kikao kazi hicho kimehusisha viongozi mbalimali kutoka wizara ya kilimo,Ardhi,Madini,Afya,Maendeleo ya jamii,Ujenzi,Mambo ya Ndani pamoja na wizara ya Nishati lengo ni kuhakikisha kila wizara inatoa elimu kwa wananchi hususani wanawake katika wiki ya mwanamke kuelekea kilele cha maadhimisho Machi 8 mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments

MAGAZETI

NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI