Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MADIWANI katika halmashauri ya manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma wameutaka uongozi wa halmashauri hiyo kupeleka pesa za uendeshaji wa ofisi kwenye ofisi za watendaji wa kata kwani kutopelekwa kwa fedha hizo kumezifanya ofisi hizo kutekeleza majukumu yake katika hali ngumu.
Sambamba na hilo Diwani huyo alisema kuwa pia kumekuwepo na changamoto kubwa ya kupelekwa kwa fedha za kushughulikia changamoto zinazowasilishwa na kata ikiwemo ambazo zimepitia kwenye baraza hilo ambapo changamoto nyingi zinachukua miaka mingi kufanyiwa kazi hivyo kuondoa umuhimu wa kuwepo kwa baraza hilo.
Kwa upande wake diwani wakata ya Kibirizi, Hamisi Ruhiso alisema kuwa Pamoja na kutopelekwa kwa fedha za uendeshaji wa ofisi (OC’s) alisema kuwa bado pia ipo changamoto ya kupelekwa kwa fedha za kumalizia miradi hivyo ametaka badala ya halmashauri kuanzisha miradi mipya ni vizuri kutoa fedha kumalizia miradi ambayo inatekelezwa.
Akihitimisha mjadala huo Naibu Meya wa manispaa ya Kigoma Ujiji,Mgeni Kakolwa alisema kuwa kikao cha baraza la madiwani kianchozungumzia taarifa za kata ni muhimu na ndiyo maana madiwani wakaomba kiwepo isipokuwa kumewakuwa na changamoto ya taarifa zinazowasilishwa kutoshughulikiwa kwa haraka hivyo ameitaka halmashauri kuona umuhimu wa taarifa na changamoto zinazowasilishwa kufanyiwa kazi kwa haraka.
Akizungumza kwa niaba ya halmashauri hiyo Kaimu Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji, Kajanja Lawi alisema kuwa wamekuwa wakizifanya kazi taarifa na changamoto zinazowasilishwa na madiwani kupitia baraza hilo la kata na kwamba upatikanaji wa fedha ndiyo umekuwa changamoto ya kufanya taarifa hizo kuchelewa kufanyiwa kazi na kwamba halmashauri italichukua jambo hilo kwa uzito na kulirekebisha.
0 Comments