Header Ads Widget

BARAZA LA NACONGO MKOA WA IRINGA LATAMBUA MCHANGO WA AIDAN MLAWA

 






Katika kuthamini juhudi za wadau wa maendeleo mkoani Iringa, Baraza la Mashirika Yasiyo ya Kiserikali (NACONGO) mkoa wa Iringa limemtambua na kumpongeza Aidan Mlawa kwa mchango wake mkubwa katika kusaidia maendeleo ya jamii. 

Mwenyekiti wa NACONGO mkoa wa Iringa, Fidelis Filipatali akizungumza katika kipindi Cha Tanzania ya Leo kinachorushwa na Matukio Daima Tv alisema kuwa Mlawa ni mmoja wa wadau muhimu wa maendeleo ambao wamekuwa mstari wa mbele kusaidia jitihada za serikali na asasi mbalimbali katika kuinua hali ya maisha ya wakazi wa Iringa.

Kwa mujibu wa Filipatali, licha ya kuwa Mkazi wa Wilaya ya Kilolo, Mlawa amejitoa kusaidia maendeleo ya wilaya zote za mkoa wa Iringa kwa hali na mali.

Kutokana na mchango wake wa kipekee, NACONGO Iringa, katika kikao chake cha maandalizi ya mkutano mkuu, kimemteua kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano huo utakaofanyika tarehe 20 Februari mwaka huu katika Wilaya ya Kilolo.

Kuwa kwa muda mrefu, Aidan Mlawa amekuwa akijitolea kusaidia  jamii mkoani Iringa, hususan katika nyanja za elimu, afya, mazingira, na maendeleo ya vijana na nyumba za ibada.


Kuwa mchango wake umekuwa wa manufaa makubwa kwa jamii, na kwa sababu hiyo, Baraza la NACONGO limeona ni vyema kumtambua na kumtunuku tuzo ya heshima kama shukrani kwa juhudi zake.

 Filipatali alisema kuwa Mlawa amekuwa akishiriki katika kuchangia vifaa vya shule kwa wanafunzi wanaotoka katika familia zenye hali duni, kusaidia miradi ya maji safi na salama, pamoja na kuhamasisha vijana kushiriki katika shughuli za maendeleo na ujasiriamali. 

Kazi zake zimeleta mabadiliko chanya na zimechochea juhudi za mashirika mengine katika kuboresha maisha ya wakazi wa Iringa.

“Kama NACONGO Mkoa wa Iringa, tunatambua mchango wa wadau wa maendeleo na tunajivunia kuwa na watu kama Aidan Mlawa ambao wanajitoa kwa dhati kusaidia jamii hii ndiyo sababu tumeamua kumteua kuwa Mgeni Rasmi wa mkutano wetu mkuu na kumtunuku tuzo ya heshima,” alisema Filipatali.

Baraza la NACONGO Mkoa wa Iringa limekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na serikali na wadau wengine wa maendeleo katika kuboresha huduma za kijamii. 

Kwa muda mrefu, NACONGO imekuwa ikifanya kazi kwa ukaribu na mashirika yasiyo ya kiserikali, sekta binafsi, na wadau wa maendeleo ili kuhakikisha kuwa miradi inayotekelezwa inaleta tija kwa wananchi.

Kwa mujibu wa viongozi wa NACONGO, kazi inayofanywa na Aidan Mlawa inaendana na malengo ya baraza hilo katika kuhakikisha jamii ya Iringa inapata maendeleo endelevu. 

Akielezea uhusiano wa karibu kati ya NACONGO na wadau wa maendeleo kama Mlawa kuwa umekuwa na mchango mkubwa katika kusaidia kutatua changamoto zinazoikabili jamii, kama vile ukosefu wa huduma bora za afya, elimu, na ajira kwa vijana.

Katika mkutano mkuu wa Februari 20, mbali na Mlawa kuwa Mgeni Rasmi, viongozi wa serikali, wawakilishi wa mashirika ya maendeleo, na wadau wengine muhimu watashiriki katika kujadili njia bora za kuendeleza maendeleo ya Iringa. 

Alisema kuwa Lengo kuu la mkutano huo ni kuboresha ushirikiano kati ya serikali, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wadau wa maendeleo kwa ajili ya ustawi wa jamii.



Katika kuthamini mchango wake mkubwa kwa jamii, NACONGO Mkoa wa Iringa imetangaza kuwa Mlawa atatunukiwa tuzo maalum ya heshima. Tuzo hiyo inatolewa kwa watu waliotoa mchango mkubwa katika kuboresha maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo.

“Tuzo hii ni ishara ya shukrani na kuthamini juhudi za watu wanaojitoa kwa dhati kuleta maendeleo kwa jamii zao. Aidan Mlawa ni mfano wa kuigwa, na tunatarajia kuona watu wengi zaidi wakifuata nyayo zake katika kujenga taifa lenye maendeleo na ustawi,” alisema Filipatali.

Tuzo hiyo itakabidhiwa rasmi katika mkutano mkuu wa NACONGO Mkoa wa Iringa, ambapo viongozi wa serikali NaconGo Taifa na wadau wa maendeleo watakuwa mashahidi wa heshima hiyo.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI